Monday, 21 November 2016

Wasifu wa Trump, mshindi wa urais Marekani

Donald Trump, rais mteule wa Marekani ambaye anatarajiwa kuapishwa tarehe 20 Januari mwaka 2017, ni tajiri anayemiliki majumba mengi na ambaye amekuwa mtangazaji wa kipindi cha maisha ya uhalisia kwenye runinga.
Amekuwa mtu anayeangazia sana ushindi katika maisha yake na alikuwa tangu mwanzo amesema ni lazima afanikiwe katika kupata tuzo kuu duniani, kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani.
Kwa wafuasi wake, ndiye anayeweza kuleta ufanisi kwa Marekani.
Kwao, huyu ni tajiri shupavu anayeweza kusuluhisha matatizo yote ya nchi ambayo wanahisi yameshusha hadhi ya Marekani duniani.
Wengi wao ni raia wa Marekani wafanyikazi hasa wenye asili ya Kizungu na walio na maisha ya kadri.
Mbaguzi na mfitini
Hata hivyo kwa wakosoaji wake, walisema huyu ni mbaguzi na mfitini, mfidhuli mkubwa ambaye angepokeza ushindi kwa Hillary Clinton au kuitumbukiza dunia kwenye janga kubwa. Walinoa kwa hilo la kwanza kwani alimshinda Bi Clinton kwa urahisi katika uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Novemba.

Obama: Sitanyamaza wakati wa utawala wa Trump

Bw Obama na Bw Trump walikutana White House siku mbili baada ya uchaguzi
Rais wa Marekani anayeondoka Barack Obama amesema huenda akazungumza, kinyume na utamaduni wa siasa Marekani, iwapo mrithi wake Donald Trump atatishia "maadili muhimu" ya Marekani.
Huwa desturi kwamba marais wa zamani wa Marekani huwa hawajiingizi sana katika siasa baada ya kuondoka madarakani na huwa hawazungumzi kuhusu warithi wao.
Akiongea katika kikao na wanahabari wakati wa mkutano wa nchi za Asia na Pasifiki (Apec) mjini Lima, Peru, Bw Obama amesema anakusudia kumsaidia Bw Obama na kumpa muda wa kueleza maono yake.
Lakini amesema kwamba, kama raia, huenda akalazimika kuzungumza kuhusu baadhi ya mambo.

Wednesday, 2 November 2016

Alicho kizungumza Rais Magufuli kuhusu mikopo ya elumu ya juu na watoto wa vigogo wanao pata mikopo.