Labels

Sunday, 30 April 2017

Mbao fc yaivua Ubingwa Yanga


Klabu ya soka ya Mbao fc ya jijini Mwanza nchini Tanzania Jana imefanikiwa kuwafunga Mabingwa wa soka Tanzania bara na Kombe la Shirikisho Tanzania klabu ya Yanga Bao 1-0 kwa bao la kujifunga kupitia kwa Vincent Andrew 'Dante' na kutinga hatua Fainali .
Hivyo kwa matokeo hayo sasa Mbao fc mwishoni mwa juma hili watakutana na Simba Sc katika hatua ya fainali.
Simba sc Klabu wao walifanikiwa kutinga fainali ya michuano hiyo kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam fc , Mshindi wa Kombe hili ndie atakayeiwakilisha Tanzania Bara katika Mashindano ya Kombe la Shirikisho kwa Msimu ujao.

Soma hapa kujua ni nafasi ngapi za kazi serikali ime tangaza.

Serikali kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia watanzania  wenye sifa na uwezo kujaza jumla ya nafasi wazi za kazi 2,748 kwa ajili ya waajiri mbalimbali Nchini.
Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi nafasi hizo za kazi ambazo zinapatikana katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz ni kwa ajili ya waajiri mbalimbali wa Ofisi za Umma.
Daudi alitaja nafasi za kazi zinazotangazwa kuwa ni Afisa Uvuvi daraja la ii, Mvuvi msaidizi daraja la ii, Afisa Mifugo msaidizi daraja la ii, Afisa mifugo daraja la ii, Mteknolijia wa samaki daraja la ii, Daktari wa mifugo daraja la ii,Afisa utafiti Mifugo daraja la ii, Daktari utafiti Mifugo daraja la ii, Fundi sanifu Maabara Mifugo daraja la ii, Mkufunzi Mifugo daraja ii, Mkufunzi wa Mifugo msaidizi na Daktari Mifugo.
Kada nyingine ni Mkufunzi daraja la ii, Mtekinolojia wa Samaki msaidizi daraja la ii, uunda boti daraja ii, nafasi 2, Dereva wa vivuko daraja la ii, msaidizi mifugo,afisa kilimo daraja la ii, Afisa kilimo msaidizi daraja la ii, Mhandisi kilimo daraja la ii, Fundi sanifu daraja la ii, Afisa utafiti kilimo daraja la ii, Mkufunzi wa kilimo msaidizi, Afisa kilimo msaidizi daraja la iii,Dereva daraja la ii, mlinzi, Mhasibu mkuu daraja ii, Msanifu lugha mkuu iii  na Afisa vipimo.

Aina ya simu za smartphone kudhibiti kisukari

Simu moja aina ya smartphone imechukuwa jukumu muhimu katika majaribio ambayo huenda yakawasaidia mamilioni ya watu duniani ambao wanakabiliwa na ugonjwa wa kisukari kuweza kuthibti kiwango cha sukari.

Watafiti wa China katika jarida la sayansi wanasema walivumbua seli za insulini na kuzidunga ndani ya panya ili kufanya kazi wakati zinapoangazwa na mwanga wa LED.
Mwanga huo ulizalishwa na programu ya simu hiyo aina ya smartphone baada ya kupokea data kutoka kwa kifaa cha kupimia damu ilio na sukari ndani ya panya huyo.
Kwa sasa watu walio na kisukari hupimwa damu ili kubaini ni wakati gani wanahitaji sindano za insulini.

Friday, 28 April 2017

Korea Kaskazini ‘yashindilia msumari’ baada ya Marekani kupeleka Meli za Kivita


Serikali ya Korea Kaskazini imetoa tamko la msimamo mkali kufuatia hatua ya Marekani 
kusogeza meli zake za kivita katika rasi ya nchi hiyo siku chache zilizopita.
Nchi hiyo imetangaza kuwa inaendelea na mpango wake wa kufanya jaribio kubwa zaidi la bomu na makombora ya nyuklia litakalokuwa la sita na kwamba hawatakoma hata kama Marekani itaendelea na mipango yake ambayo wamedai ni ya chuki.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki za Binadamu kwenye Chuo cha Jamii cha Korea Kaskazini aliyepewa mamlaka ya kuzungumzia masuala ya mgogoro wa nchi hizo mbili, Sok Chol Won jana aliiambia CNN kuwa mpango huo kabambe uko palepale.
“Majaribio ya mabomu na makombora ya nyuklia ni muhimu kwetu kama sehemu ya juhudi za kuimarisha nguvu zetu za nyuklia,” alisema.
“Wakati ambapo Marekani inaendelea na hatua zake za chuki na hasira, majaribio ya nyuklia na makombora hayatakoma,” alisisitiza.
Kauli hiyo imekuja wakati ambapo Baraza la Mawaziri la Marekani limeweka msisitizo wa kuiwekea Korea Kaskazini vikwazo vya kiuchumi na kidiplomasia huku ikitoa wito pia wa kuwepo kwa mazungumzo.
Hata hivyo, Rais Donald Trump na Makamu wake wamesisitiza uwezekano wa kuwepo hatua za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini.

Serena: Nilionyesha mimba yangu kimakosa

Serena Williams amesema kuwa alifichua kuhusu mimba yake kimakosa baada ya kuweka picha kwa Snapchat.
Serena Williams amesema kuwa alifichua kuhusu mimba yake kimakosa baada ya kuweka picha kwa Snapchat.
Bingwa huyo wa taji la Grand slam mara 23 alichapisha picha katika mtandao huo wa kijamii akijiangalia katika kioo akiwa ameandika ujumbe wiki 20 kabla ya kufuta kabla ya wasimamizi wake kuthibitisha habari hizo.
Williams mwenye umri wa miaka 35 alisema kwamba alipiga picha kila wiki ili kufuatialia mimba yake.
''Nilikuwa nikijihifadhia'', alisema.
''Nilikuwa nikiendelea vizuri lakini bahati mbaya picha moja nikaichapisha katika Snapchat''.
Bingwa huyo nambari moja kwa upande wa wanawake anatarajiwa kujifungua majira ya vuli, akisema kua aligundua kwamba ana mimba siku mbili kabla ya mashindano ya Australia Open mnamo mwezi Januari.
Williams mwenye umri wa miaka 35 alisema kwamba alipiga picha kila wiki ili kufuatialia mimba yake.


Guardiola: Sijui kama Bravo atatuchezea tena



Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema hafahamu iwapo mlindalango wa klabu hiyo Claudio Bravo ataweza kucheza tena baada ya kuumia wakati wa mechi kati ya City na Manchester United Alhamisi.
Bravio, 34, aliondolewa uwanjani kwa machela baada ya kuumia akijaribu kuondosha mpira kutoka eneo la hatari wakati wa mechi hiyo ya Ligi ya Premia.
Willy Caballero aliingia nafasi yake.
"Bila shaka ni jeraha, labda litamuweka nje wiki kadha," alisema Guardiola,
"Sijui kama ataweza kucheza tena msimu huu."
Sare hiyo tasa, ambayo Bravo aliondoka uwanjani dakika ya 79, ilikuwa mechi yake ya sita kucheza kati ya 22 alizocheza Ligi ya Premia bila kufungwa tangu anunuliwe £15.4m kutoka Barcelona.

Mourinho Sergio aguero alitumia werevu baada ya kugongwa kichwa na Marouane Fellaini.




Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema Sergio Aguero alitumia werevu baada ya kugongwa kwa kichwa na Marouane Fellaini.
Fellaini, 29, alioneshwa kadi nyekundu moja kwa moja dakika ya 84, sekunde chache baada yake kuoneshwa kadi nyingine ya manjano kwa kumtega nyota huyo wa Argentina.
Mechi hiyo ya Ligi ya Premia ilimalizika sare tasa.
"Sikutazama tukio hilo lakini naweza kufikiria kwamba labda kadi nyekundu na ilitokana na uchezaji wa uzoefu, na ujanja kiasi wa mchezaji huyo wa Argentinia," alisema Mourinho.
Alipoulizwa iwapo kiungo wa Ubelgiji Fellaini hakutumia busara, Mourinho alisema: "Marouane anasema ilikuwa kadi nyekundu kwa sababu yeye ni Marouane.
"[Mwamuzi] Martin Atkinson aliniambia kwa maoni yake ilikuwa kadi nyekundu, lakini nilimuona Aguero baadaye na hakuwa ameumia pua, hakuwa na jeraha kichwani, na uso wake ulikuwa na tabasamu kama kawaida. Sina uhakika…
"Iwapo Sergio hangejiangusha basi bila shaka haingekuwa kadi nyekundu, lakini Marouane alimpa fursa ya kufanya hivyo ….Sijui, lakini ninachokifahamu ni kwamba tulicheza dakika 15 na wachezaji 10 na vijana wetu walicheza vizuri sana, walipigania kuondoka na alama moja."
Felliani sasa amefukuzwa uwanjani mara tatu tangu ajiunge na United kutoka Everton kwa £27.5m mwezi Septemba 2013.
Awali, alifukuzwa uwanjani wakati wa mechi iliyomalizika sare tasa na Hull City mnamo 24 Mei 2015 na mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Real Sociedad mwezi Novemba 2013.
Fellaini pia alifukuzwa wakicheza mechi iliyomalizika sare 1-1 akichezea Everton dhidi ya Bolton katika Ligi ya Premia 2010.

Thursday, 27 April 2017

Man city na Mashetani wekundu man united watoka sare.






Mchezo wa dabi ya jiji la Manchester kati ya Mashetani wekundu wa Man United na Man City umemalizika kwa sare ya bila kufunga mchezo huo ulipigwa katika dimba la Etihad.
Kutoshana nguvu kwa timu hizi kunafanya vita ya kuwania nafasi nne za juu kuendelea kuwa kali City wako nafasi ya nne kwa alama 65 alama moja mbele ya United walioko nafasi ya tano kwa alaam 64.
Man city wakiwa wenyeji wa mchezo huo waliutawala mchezo kwa asilimia kubwa na umiliki wa mpira ukiwa ni asilimia 69 kwa 31.
United walibaki pungufu katika dakika ya 84 baada ya kiungo wake Marouane Fellaini kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje kwa kadi nyekundu, baada ya kumpiga kichwa Sergio Aguero.Huu ulikua ni mchezo wa 24 kwa Man united wakicheza bila kupoteza msimu huu

Wednesday, 26 April 2017

Suruali chafu zauzwa dola 425

Wengi katika mitandao ya kijamii wameishutumu kampuni hiyo ya mavazi

Kampuni moja ya mavazi nchini Marekani imeshutumiwa vikali kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutangaza kwamba inauza suruali za jeans zilizo na uchafu kwa $425 (£330; €390).
Kampuni ya Nordstrom imezipa suruali hizo jina Barracuda Straight Leg.
Suruali hizo zimebandikwa matope yaliyokauka.
Jeans hizo zimeelezwa na mtandao wa Nordstrom kuwa kiashiria cha maisha magumu ya Wamarekani wafanyakazi na pia dhihirisho la kutia bidii kazini.
Lakini wakosoaji kwenye Facebook wamesema mavazi hayo ya kampuni hiyo yanasikitisha.
"Unaweza kupata sura sawa kwa kutumia pesa kidogo sana, kwa kujigaragaza kwenye shamba lako au kwenda shambani kulima na kupalilia mimea au maua," mmoja alisema.
Mtangazaji wa kipindi cha Dirty Jobs katika runinga ya Discovery Channel Mike Rowe amesema suruali hizo "zinaonekana kama zimevaliwa na mtu aliyefanya kazi yenye uchafu mwingi" lakini "zimeshonewa watu wasiogusa uchafu".
Nordstrom imesema mavazi hayo yamepakwa matope maalum na kukaushwa na lengo ni kuonyesha kwamba anayeyavalia hana wasiwasi wa kupata uchafu akifanya kazi yoyote ile.
Nipe jeans zako kisha uniongezee dola 200, nitakuandalia vazi lako. Unaweza kuamua iwapo unataka uchafu wa kinyesi cha farasi au kuku, grisi kutoka kwenye trekta au udongo wa mfinyanzi... na kwa $600 nitampa mbuzi atafune jeans zako na kutoboa mashimo," aliandika mmoja wa wakosoaji.
Lakini kunao wengine waliosema iwapo kuna watu wanaoweza kulipa $400 kununua mavazi hayo machafu, basi nawalipe.
Mwezi jana Nordstrom walianza kuuza jeans zenye 'dirisha magotini' ambazo zinauzwa $95 (£74; €87) .

Mhalifu mtanashati zaidi azuiwa kuingia Uingereza



Jeremy Meeks, ambaye wakati mmoja alijizolea sifa za kuwa "mhalifu mtanashati zaidi duniani", amezuiwa kuingia Uingereza.
Mwanamitindo huyo alivuma sana mtandaoni mwaka 2014 picha yake ilipopakiwa kwenye mtandao.
Taarifa zinasema alijaribu kuingia Uingereza kwa shughuli za kikazi.
Maafisa wa uhamiaji walimzuia Jumanne katika uwanja wa ndege wa Heathrow, London na tayari amesafirishwa kurejeshwa Marekani.
Maafisa wa wizara ya mambo ya ndani wameambia BBC kwamba wanafahamu kuhusu kisa hicho, lakini hawawezi kuzungumzia kisa cha mtu binafsi.
Hata hivyo, kifungu 320 cha sheria za uhamiaji za Uingereza kinasema maafisa wa uhamiaji uwanja wa ndege au mpakani wanaweza kumzuia mtu yeyote ambaye amefungwa jela kati ya miezi 12 na miaka minne kuingia Uingereza.
Mtu kama huyo hata hivyo hawezi kuzuiwa miaka 10 baada yake kumaliza kutumikia kifungo.
Sheria hiyo ni miongoni mwa masharti mengine yanayoweza kutumiwa kuzuiwa watu waliofungwa jela mataifa ya nje kuingia Uingereza.

Jeremy Meeks alishtakiwa kosa la kuwa na bunduki 18 Juni 2014 na akafungwa jela hadi Machi mwaka jana.
Awali, alikuwa ametumikia kifungo cha miaka tisa kwa kosa la wizi kuanzia 2002 hadi 2011.
Jeremy amekuwa akitafutwa sana na kampuni za mitindo ya amvazi.
Meneja wa Jeremy, Jim Jordan, ameambia Daily Mail kwamba mwanamitindo huyo alikuwa amebeba stakabadhi zifaazo pamoja na barua kutoka kwa afisa wa kumfuatilia mfungwa anayetumikia kifungo cha nje.
Jeremy anadaiwa kutia saini mkataba na kampuni ya White Cross Management siku chache baada ya kuondoka jela mwaka jana.
Alishiriki maonesho ya mitindo mara ya kwanza Wiki ya Mitindo ya New York mwezi Februari.
Picha yake iliyopakiwa na polisi wa Stockton ukurasa wao wa Facebook 2014, imependwa zaidi ya mara 101,000 na kusambazwa mara 12,600.

Barca, Madrid zapeta La Liga



Miamba ya soka la Hispania vilabu vya Barcelona na Real Madrid vimendelea kutamba katika ligi hiyo kwa kupata ushindi wa mabao mengi katika michezo yao.
Barcelona waliichapa timu inayoburuza mkia katika ligi Osasuna, kwa mabao 7 -1 mabao ya Barca yakifungwa na Lionel Messi aliyefunga mabao mawili, Andre Gomes, nae akafunga mawili kinda Francisco Alcacer, akatupia nae magoli mawili huku Javier Mascherano, akifunga bao moja.

Real Madrid wakiwa ugenini katika dimba la Municipal de Riazor, waliwafunga Deportivo La Coruna, kwa mabao 6-2, mabao ya Real yalifungwa na James Rodriguez, aliyefunga mara mbili na mengine yakifungwa na Alvaro Morata, Lucas Vazquez, Isco na kiungo Casemiro
Leganes wakashinda kwa 3 - 0 dhidi ya Las Palmas, Nao Valencia wakalala nyumbani kwa kufungwa 3-2 na Real Sociedad.

Arsenal, Tottenham zashinda Epl


Mshike mshike wa kuwania ubingwa wa ligi kuu England umeendelea kushika kasi ambapo Tottenham Hotspur walipata ushindi ugenini wa bao 1-0 dhidi ya Crystal Palace.
Bao pekee la Spurs katika mchezo huo lilifungwa na kiungo Christian Eriksen, katika dakika ya 78 ya mchezo na hivyo kuendelea kuwakimbiza vinara wa ligi hiyo Chelsea, wanaongoza ligi kwa alama 78 huku Spurs wakiwa nafasi ya pili kwa alama 74.
Nao washika mititu wa London Arsenal, walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Leicester City, bao la kujifunga la beki wa Leicester Robert Huth, ndio liliwapa vijana wa Wenger alama tatu muhimu na kusogea mpaka nafasi ya sita katika msimamo wa ligi.
Vibonde wa ligi Middlesbrough wakautumia vyema uwanja wa nyumbani wa Riverside kuwa kuwachapa kwa bao 1-0 vibonde wengine wa ligi Sunderland ambao ndio wanaburuza mkia katika ligi hiyo.

Arsenal kucheza dhidi ya leicester


Arsene Wenger akiishangilia timu yake baada ya kuibandua Manchester City katika kombe la FA
Mshambuliaji wa Arsenal Alex Oxlaide Chamberlain huenda akashiriki katika mechi dhidi ya Leicester City Licha ya kuondoka katika uwanja wa Wembley baada ya mechi ya Jumapili ya FA akiuguza jeraha.
Kiungo huyo wa kati aligongwa katika mguu lakini kcha Arsene Wenger anasema kuwa alichukua hatua ya tahadhari.
Mchezaji wa Leicester Wes Morgan anauguza jereha la mguu huku msimu wa Nampalys Mendy ukikamilika baada ya kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu.
Beki Robert Huth anarudi baada ya kuhudumia marufuku ya ligi ya klabu bingwa ,lakini Slimani anaendelea kuuguza jeraha.

Wenger: Sitamuuza Sanchez kwa wapinzani wangu

Sanchez
Mshambuliaji wa Arsenal Alexi Sanchez hatouzwa kwa kilabu ya ligi ya Uingereza kulingana na mkufunzi Arsene Wenger.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kutoka Chile, ambaye alifunga bao la ushindi katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Manchester City ana mwaka mmoja uliosalia katika kandarasi yake lakini bado hajatia saini kandarasi mpya.
''Sidhani kama unaweza kumuuza kwa klabu yoyote ya Uingereza, huo ni ukweli'', alisema Arsene Wenger.
''Lakini kama nilivyosema ,nadhani atasalia na kuweka saini kandarasi mpya''.
Wenger bado hajathibitisha iwapo atasalia katika klabu hiyo ya London kaskazini, lakini anasema anafanya kazi ya kuwasajili wachezaji wapya msimu ujao.
Kandarasi ya raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 67 inakamilika mwishoni mwa msimu na amepewa kandarasi mpya.
''Nafanya kazi hadi siku ya mwisho ya msimu'', alisema Wenger mwenye umri wa miaka 67.
''Wachezaji wanaonunuliwa ndio mpango wa kila klabu katika siku zake za usoni'' ,alisema Wenger.
''Swala la iwapo nitasalia au la sio muhimu kwa sasa, kilicho muhimu ni siku za usoni za klabu hii'',Wenger alisema mnamo mwezi Februari kwamba ataamua kuhusu kandarasi mpya mnamo mwezi Machi ama Aprili na baadaye kutangaza.
''Najua nitakachofanya na hivi karibuni mutajua''.

Tuesday, 25 April 2017

United Airlines wachunguza kifo cha sungura mkubwa

Sungura wakubwa huwa na thamani.
Shirika la ndege la United Airlines linachunguza kifo cha sungura mmoja mkubwa aliyefariki alipokuwa akisafirishwa kwenye moja ya ndege za shirika hilo.
Sungura huyo kwa jina Simon, aliyekuwa na urefu wa sentimeta 90, alipatikana amefariki

Tumbo la bandia labuniwa Marekani

kijusi kikiwa katika tumbo la bandia
Wanasayansi nchini Marekani wamebuni tumbo bandia la kutengeneza ambalo katika siku zijazo linaweza kutumiwa kuwekea watoto wanaozaliwa kabla ya muda wao, maarufu kama njiti.
Kifaa hicho ambacho kipo katika mfumo wa tumbo kimejaribiwa kwa mimba ya kondoo.

Chelsea waendelea ku kimbiza ligi baada ya kuichapa Southampton.

Eden Hazard akifunga bao la kuongoza
Klabu ya Chelsea The Blues wameendelea na wimbi la ushindi katika vita ya kuwania ubingwa ligi kuu ya England baada ya kuichapa Southampton kwa 4-2.
Nyota wa timu hiyo Eden Hazard alianza kuiandikia timu yake bao la kuongoza katika dakika ya 5 ya mchezo , katika dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza beki Gary Cahill akafunga bao la pili.

Simba yaamua kukaa kimya

Uongozi wa Klabu ya Simba umesema hauwezi kuzungumzia kitendo cha wao kupokonywa pointi tatu na Kamati ya Sheria, katiba na Hadhi za wachezaji mpaka hapo watakapopewa nakala ya maamuzi ya kikao cha kamati hiyo.
Makamu wa Rais wa Simba, Godfrey Nyange (Kaburu) alisema wamesikia taarifa kupitia mitandao na vyombo mbalimbali vya habari kuwa wamepokwa pointi walizopewa na Kamati hiyo.
''Habari hizo zilizotolewa na viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambazo zinaonesha kutokuzingatia kanuni na taratibu katika kupokonya pointi zetu kiukweli zina mapungufu makubwa''.alisema Kaburu
Aidha Kaburu, alisema kuwa wanashangazwa na kitendo cha katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Selestine Mwesigwa kukiri kuwa Mchezaji wa Kagera Sugar Fakh Mohammed, alikuwa na kadi tatu hivyo kuamua kuinyang'anya Simba pointi kutokana na kutotimiza baadhi ya vigezo wakati wa kudai haki yao.
Alisema wanashangaa kuona TFF inashindwa kutimiza majukumu yao wenyewe pasipo kusubiri klabu ziende kupeleka malalamiko na ndipo waweze kuchukua maamuzi wanayopaswa kuyachukua.
"Hili suala lipo wazi kutokana na wao wenyewe kukiri kwamba Faki, alikuwa ana kadi tatu pasipo kujali kama sisi tumekata rufaa au hatujakata, pia hatujajua ni mambo gani yanayoendelea kwa sababu mpaka hivi sasa hatujapata barua rasmi inayotueleza kile kilichofanyika kwa siku zote ambazo kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi za wachezaji walijadili kwa siku zote," alisema Kaburu.
Wakati huo huo, Katibu mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa aliitaka TFF ku badili kanuni na taratibu zinazoruhusu timu Fulani kupewa pointi za mezani endapo wanakuwa wameshindwa kupata ushindi katika Michezo yao ya awali.
Alisema kitendo cha kutoa pointi za mezani kinazidi kuzorotesha soka la Tanzania na timu ndogo ndogo zimekuwa ndio waathirika wakubwa wa vitendo hivyo.






Mwanariadha Alphonce Simbu

Balozi maalum wa DStv na Mwanariadha pekee wa Tanzania liyeshiriki mashindano ya London Marathon Alphonce Simbu amerejea nyumbani na kutoa onyo kali kwa wale atakaokabiliana nao kwenye mashindano yajayo ya dunia yatakayofanyika mwezi Agosti jijini London.
Simbu ambaye alishika nafasi ya tano katika mashindano hayo na kujishindia kitita cha dola za marekani 10,000 aliwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro na kulakiwa na maafisa mbalimbali akiwemo Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Johnson Mshana, na pia Meneja wa mwanariadha huyo Francis John

Wenger: Nimepanga wachezaji nitakaonunua

Arsene Wenger na wachezaji wake
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anasema kuwa ameanza kupanga kuhusu wachezaji atakaonunua msimu ujao licha ya kuwa hajapata thibitisho kwamba atasalia katika klabu hiyo.
Kandarasi ya Wenger inaisha mwisho wa msimu huu na tayari amepewa kandarasi mpya ya miaka miwili, ijapokuwa hajatangaza iwapo ataendelea au la.

WATAALAM WA SAYANSI WA GUNDUA KUPOTEA KWA VIUMBE WA ANGA ZA JUU.

Kiumbe wa anga za juu
Wataalamu wa masuala ya sayansi wanaotafuta maisha katika anga za juu watahitajika kusubiri zaidi
Mradi huo wa gharama ya dola milioni 100 wa kutafuta dalili za viumbe wa anga za juu bado haujapata chochote mwaka mmoja baada ya kuzinduliwa.

HABARI NJEMA KWA MASHABIKI WA RIHANA

Picha ya Rihanna na Lupita yazua mjadala wa kutengezwa kwa filamu
Picha ya Rihanna na Lupita Nyong'o imezua mjadala kwamba huenda wawili hao wanapanga kubuni filamu hatua ambayo imewashinikiza nyota hao kujitokeza na kusema ndio wana mpango huo.

Picha hiyo ya 2014 ya mitindo ilisambazwa na mashabiki wengi na sasa Rihana amesema kuwa ana mpango kama huo katika mtandao wake wa Twitter.

Vita ya kuwania ubingwa Epl kuendelea leo

Wachezaji wa Chelsea
Mshike mshike wa kuwania ubingwa ligi kuu ya England utaendelea tena leo kwa mchezo mmoja kupigwa vinara wa ligi hiyo Chelsea watakua katika uwanja wao wa nyumbani kuwaalika watakatifu wa Southampton.
Nahodha wa Chelsea Gary Cahill anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi baada ya kurejea mazoezi baada ya kupona tatizo la tumbo .
Diego Costa na Eden Hazard wanatarajiwa kuanza katika mchezo huu baada ya kuanzia bechi katika mchezo wa kombe la FA dhidi ya Tottenham wikiendi iliyopita.
Mshambuliaji hatari wa Saint Manolo Gabbiadini
Kiungo wa Southampton Oriel Romeu amereje kwenye kikosi cha timu yake baada ya kufungiwa michezo miwili iliyopita, Sam McQueen is ataukosa mchezo huo akisumbuliwa na maumivu.
Chelsea wanaongoza ligi kwa alama 75 wakiwa wamecheza michezo 32 wakifuatiwa na Tottenham wenye alama 71 kwa michezo 32.