Tofauti na unyayuaji vyuma vizito, zipo njia nyingine za kukuza misuli
na kufanya mwili kuwa katika hali ya mvuto kuliko hata ya myanyua vyuma,
na kuufanya mwili kujijenga kwa usawa bila kuwa na utofauti wa ukubwa
wa misuli ambao wanyanyua vyuma vizito wengi wao walivyo, haya hapa ni
mazoezi kumi na matano yatakayokuweka vizuri kiafya na kimuonekano..
.
Ni zoezi linalopanua kifua, kujenga kifua, kukuza misuli ya
mikono ya ndani na nje na ni zoezi zuri la kuanzia, kama unataka kuwa na
mwili wa kujijenga vizuri anza na hili zoezi.
Pull
ups inafanyisha kazi kila misuli mwilini, hasa misuli ya mikono na
mgongo, ukitaka uwe na nundu za mikono kama za Jean Claud Vandame hili
ndo hasa zoezi lako.
Ukishikilia hili zoezi bila kutingishika kwa dakika kadhaa, wewe kweli
utakua una nia na kuubadilisha mwili wako liwe hekalu la mvuto. Zoezi
hili linahitaji mabega yaliyoshiba na linafanyisha kazi misuli ya
mikono, kiuno, mgongo, shingo na miguu na zoezi hili lina zawadi moja,
linafanya tumbo lako likatike mara sita.
- Roll Out
Hili zoezi linafanana na la nusu push up(Plank), ila
linachobadilisha ni kusukuma nondo kuelekea mbele na kurudi, na jinsi
unavyoendelea kusukuma nondo ndo ambavyo zoezi linavyozidi kuwa gumu,
kwa hio unahitaji nia na kujitoa kweli, faida zake linajenga misuli ya
mgongo, kiuno, kifua na kutanua mabega.
- Glute bridge
Zoezi hili linajenga mgongo na misuli yote inaouzunguka, ukiwa
mkufunzi wa hili zoezi kinachofuata ni kuombwa namba tu na wasichana.
- Iverted Row
Hili zoezi ni la mgongo, fuata kama picha inavyolionyesha, faida
zake linafanya kifua kiwe kipana zaidi na mikono iwe na stamina zaidi.
- Close Hands Push ups
Hili zoezi ni kwa ajili ya mikono, na ni kwa ajili ya nundu za ndani
na nje ya mikono, na misuli yako inakua inakua kwa pamoja bila
kutegeana, fanya hili zoezi na utaona mabadiliko makubwa kwenye mikono
yako.
- Star Plack
Hili zoezi kidogo ni zito kidogo, na zoezi hili linalenga kifua na
mabega pamoja na misuli ya miguu na mikono, na ni zuri kwa kukata tumbo.
- Burpee
Zoezi la kupunguza mafuta mwilini, zoezi hili linafanya mwili mzima
uchemke kwa pamoja, ukiwa unafanya hili, unakua unafanyisha kazi kila
kiungo cha mwili na kuondoa sehemu dhaifu mwilini.
- Dip
Zoezi la misuli ya nyuma ya mkono na linasaidia pia kwenye misui ya
kifua na upanuaji wa mabega na kufanya kifua kikae vizuri, zoezi hili
linahitaji nia na nguvu ili lifanyike kwa mpangilio unaotakiwa na
linamzidi yule aliyelala kwenye benchi akinyanyua vyuma vizito.
- Bulgaria Split Squart
Kichura chura cha mguu mmoja nyuma, kinafanyisha kazi misuli ya
mapajani na kukufanya uwe na stamina zaidi, ukifanya hili kwa wiki
kadhaa, kama kichura chura cha kawaida kilikua kinakupiga chenga basi
utakua unafanya mara mbili ya zaidi ulivyokua unafanya.
- Suspended Push ups
Push ups ni nzuri, ila ukiiongezea ugumu kidogo kwa kuiongezea
suspenda, ni njia mojawapo ya kuiongezea misuli uzito, na kufanya iwe
misuli yenye ujazo na ya muda mrefu tofauti na yule anaebeba vyuma
vizito.
- Prone Back Extension
Hili zoezi linahimalisha kiuno, tumbo na mgongo kwa ujumla.
- Pike Push ups
Ukiwa mkongwe wa push ups, hili ndilo zoezi la mwisho la push ups na
linasaidia kuimalisha mabega na kuongeza ubora wa viazi vyako vya
mikono.
- Swiss Ball Rollout
Zoezi linavyozidi kuwa gumu ndo misuli inavyozidi kuongezeka,
ukiweza kuzingatia haya mazoezi utajishangaa baada ya wiki tatu
mfululizo ukiwa unayafanya.
No comments:
Post a Comment