Labels

Wednesday, 26 October 2016

Mtu aliyevalia kama mti akamatwa Marekani

Tree guy

Mwanamume mmoja nchini Marekani, ambaye ameanza kufahamika kama "binadamu mti", alikamatwa baada yake kuvuka barabara akiwa amevalia kama mti.

Asher Woodworth, kutoka jimbo la Maine nchini Marekani, alijifunika kwa matawi na kuvuka barabara polepole.
Polisi walimsindikiza hadi kando mwa barabara kabla ya kumuweka kizuizini.
Asher baadaye aliachiliwa huru na polisi.
Aliambia BBC kwamba alikuwa akivuka barabara mara ya tatu pale alipokabiliwa na maafisa wa polisi.
Yeye ni mwigizaji mjini Portland, Maine.
Anasema: "Nilipata wazo hili nilipokuwa natafakari sana siku moja."
Anasema alikuwa anataka tu kuwashangaza watu kwa mavazi yake na kuwafanya "watafakari upya kuhusu matarajio yao".
Alikuwa ametumia matawi ya miti ya aina mbalimbali na anasema ilimchukua yeye na rafiki yake saa kadha kukamilisha vazi hilo.


Matawi
Alikuwa amepakia picha yenye vazi jingine linalokaribiana na hilo kwenye mtandao wa Tumblr mwezi uliopita 

  •  Anasema matawi ya miti aliyokuwa amevalia yalikuwa "yananukia".
  • Lakini mbona akaamua kuvalia matawi ya miti?
  • "Huwa nahisi nina uhusiano wa karibu na miti, naipenda sana," aliambia.
  • Alikuwa pia ametiwa moyo na mpiga picha Charles Freger, aliyepiga picha hii iliyo hapa chini
  •  
    Mwanamume aliyefunikwa kwa matawi
    Image caption Asher Woodworth pia aliweka picha hii ukurasa wake wa Tumblr
Baada yake kukamatwa, Asher Woodworth anasema alikaa saa sita kizuizini kabla ya kuachiliwa huru Jumatatu.

No comments:

Post a Comment