Njia salama ya kuongeza Makalio kwa njia salama ya mazoezi.
Miaka ya hivi karibuni kua na makalio makubwa imekua ni fasheni
muhimu sana kiasi kwamba wanawake wasio na makalio makubwa wamejikuta
wakipata tabu na hata kufanya upasuaji hatari ili kuongeza makalio na
wengi wameharibika kabisa au kupoteza maisha kwenye oparesheni hizo
hatari.
Lakini kama jinsi wanaume wanavyobeba vyuma na kuongeza vifua na mikono hivyohivyo wanawake wanaweza kuongeza misuli hiyo muhimu ya makalio ambayo kitaalamu inaitwa gluteal maximus,gluteal minimus na gluteal medias. hiyo ndio misuli mikuu mitatu ambayo kwa pamoja inaitwa makalio na ikifanyiwa mazoezi vizuri huongezeka na kua mikubwa.
Ni kweli ukubwa wa makalio na kiungo chochote cha mwili hufuata ukoo lakini pia mazoezi husaidia sana kukuza makalio au kiungo chochote cha mwili chenye misuli lakini sio kua makubwa tu lakini hata kuyafanya kua na shepu nzuri na kuvutia..
Unaweza kua hujaamini bado lakini kwa kukuthibitishia habari hizi ni kwamba jeniffer lopez mwanamuziki na muigizaji wa filamu nchini marekani ambaye anaongoza kwa kua na makalio makubwa zaidi kuliko wasanii wote mpaka akayakatia bima yaani insurance anafanya mazoezi haya kama ifuatavyo..

Mazoezi ya squat; mazoezi haya huanzwa kwa kusimama na miguu
yote miwili kisha kuanza kama unakaa hewani halafu unainuka, mazoezi
haya huvuta misuli ya makalio na kuibana kisha kuongeza upana na siku za
kwanza za mazoezi haya mtu hujisikia maumivu na kuanza kuhisi nguo
zimeanza kubana mpaka mapajani. ni zoezi kuu na muhimu katika kukuza
makalio.fanya zoezi hili kwa raundi tatu kila raundi fanya mara kumi na
tano au unaweza ukaanza kama picha inavyoonyesha hapo kwa mwezi mmoja
kisha ukaendelea na mazoezi ya kawaida kama nilivyoelekeza.
zoezi la bridge; watu wengi wanashinda wamekaa kwenye viti
mashuleni au maofisini muda mwingi na hali hii hufanya hata mtu mwenye
makalio makubwa ya kuzaliwa nayo kuanza kupoteza shepu yake nzuri ya
mwanzoni. zoezi hili huanza kwa kulala chini kwa mgongo kisha inua kiuno
kwa juu, sasa bakia kwa hali hii kwa muda kisha nyoosha mguu mmoja kwa
mbele kwa sekunde kadhaa afu rudisha chini halafu badilisha mguu.fanya
hivi kwa kila mguu mara kumi kwa raundi tatu huku ukipumzika dakika
mbili kila baada ya raundi.
donkey kick; piga magoti kisha weka mikono chini kama mbuzi
anavyosimama kisha inua mguu mmoja wa nyuma mpaka uangalie juu kisha
rudisha chini taratibu.fanya hivi raundi tatu huku kila mguu ukiinua na
kuurudisha mara 20.
kula protini nyingi: vyakula vya protini ni muhimu kujenga
misuli na mifupa hivo kula sana maharage, nyama, samaki,maziwa, karanga,
korosho na kadhalika. hii itakujenga haraka sana na kukupa matokeo
mazuri kwani mwili unajengwa na chakula.
chagua aina nzuri ya wanga; ulaji wa mikaango kama chips,
chapati, maandazi na kadhalika sio wanga nzuri kwani huleta vitambi na
kukufanya ue na shepu mbaya ni vizuri kula wanga asili kama
ugali,viazi,mihogo,wali na kadhalika.
tumia mboga za majani; mboga za majani ni muhimu sana kwani
husaidia chakula ulichokula kiweze kunyonywa na mwili kirahisi na
kupunguza uwezekanao wa kupata kitambi.
tumia virutubisho vya kutosha; virutubisho vyenye madini
mbalimbali na protini ni muhimu sana kwani vyenyewe vinaenda moja kwa
moja kufanya kazi kwenye mwili na kuanza kujenga misuli hii bila kuanza
kufyonzwa taratibu tumboni kama vyakula vingine. utafiti unaonyesha
wanaotumia virutubsho hivi hufanikiwa sana kuliko wasiotumia
kabisa.jinsi ya kutumia; chota kijiko kimoja kilichowekwa kwenye
virutubisho vyako kisha changanya na maziwa kwa upande wa protein shake
na kwa upande wa argi changanya kijiko kimoja cha unga na maziwa ya
mgando au juice.kunywa mara moja au mbili kwa siku huku ukiendelea na
mazoezi.
mwisho: kama ilivyokua kwa mazoezi mengine yeyote itakuchukua
muda angalau wiki mbili au mwezi mmoja kuanza kuona matokeo na
haimaanishi kwamba ndio matokeo mazuri yakipatikana ndio unaacha hapana,
mazoezi ni muhimu kwa mwili wa binadamu, unaweza ukaanza na zoezi la
mwezi yaani mara moja kwa siku kisha endelea na zoezi hili mara tano kwa
wiki baada ya mwezi wa kwanza. kumbuka kama ilivyo kwa mazoezi mengine
ya mwili, unahitaji moyo wa mazoezi kufanikiwa, usije ukafanya zoezi
siku mbili ukaacha afu ukategemea mabadiliko..unaweza ukatutafuta kupata
virutubisho hivyo, kupata video za mazoezi na kwa msaada wa kitaalamu
zaidi.
No comments:
Post a Comment