Kuku wa kienyeji.
kujenga banda lakuku.
Unavyoanza kujenga banda la kuku kitu cha kwanza kupangilia mpangilio mzima wa mabanda yatakayo kaa:
- Upepo.
- Sehemu iwe inafikika
- Na isiwe na unyevunyevu.
Mpangilio wa mabanda.
Banda la kwanza kabisa ni banda la kuku wa nyama
ndio lina jengwa mwanzoni,kuwe na upepo wa kutosha na banda linalo fuata ni kuku wa mayai,banda la mwisho kabisa ni banda la kuku wa kienyeji hili lina jumuisha bata,bata mzinga pamoja na kanga na ndege wengine wafugwao
sababu zinazo fanya ujenzi huu wa banda bora uwe wa mpangilio ni hizi zifuatazo;
(1) Magonjwa mengi ya kuku yana ambukizwa kwa njia ya hewa hivyo huwauwa zaidi kuku wa nyama wanao wahi kutoka bandani ni rahisi kupata maambukizi kutoka kwenye kuku wanao kaa mdamrefu bandani.
(2)Kwamfano kuku wa kienyeji,bata,bata mzinga,kanga hukaa bandani mda mrefu sana hivyo magonjwa ya kuambukiza huwa wana kaanayo sana mwilini mwao kwaiyo wao wanakua wamejijengea kinga mwilini mwao tofauti na kuku wa nyama.
ULISHAJI WA KUKU WA KIENYEJI.
1)Kula kwa kuzurura(free range system)
2)kula kwa kufungwa/kwenye mabanda.
1)Njia ya kuzurura.
Kuku wanaofunguliwa tu na kuanza kutafuta chakula wenyewe njia hii ni rahisi lakini kutoa dawa kwa kulisha ni ngumu kwasababu kuku wanapo rudi jioni huwa wameshiba hivyo huwezi wapa dawa kirahisi.
2)Njia ya kufugia kwenye banda.
Njia hii ni nzuri lakini ina madhara kwa mfugaji asiye makini kwasababu inaitaji uangalizi mzuri katika kulisha chakula kwani virutubisho vingi vya kwenye chakula kuku anaye zurura anauwezo wa kujitafutia mwenyewe nakuweka uwiano wa virutubisho ndani ya mwili wenyewe.
KUZUIA MAGONJWA YA KUAMBUKIZWA WENYEWE KWA WENYEWE
1)MABORESHO YA UFUGAJI.
Kwakawaida kuku wa kienyeji huchukua miezi 5-6 kuanza kutaga mayai lakini chakula bora kimefuta mfumo huo hivyo kuku wakienyeji sikuizi huchukua miezi mi 4 na kuanza kutaga,kama utafuata ufugaji bora na chakula bora hutaga mayai 100 kwa mwaka.
MABANDA.
Mabanda yawe na hewa ya kutosha ili waweze pumua vizuri bila kushikana.
2)Waweza weka bembea ndani ya nyumba huwafanya kuku mifupa itanuke kila wanapo ruka ni mazoezi ya kujenga mwili.
3)AINA MBILI ZA KUFUGA KUKU WA/NDANI(INTENSIVE SYSTEM)
1)Berry charge system(ufugaji wa kutumia vyuma au mbao).
2)Deep litre system.
Njia ya kulisha kuku katika banda tunatakiwa maranda,majani ya mpunga/ngano,Pumba hutumika kiasi cha 12.20 za ujazo.
FAIDA ZAKE.
-Kuku wengi hufugwa katika sehemu ndogo.
-kuku hupata kinga za hali ya hewa,jua na baridi.
Pia hukingwa zaidi na wanyama wasumbufu kama mwewe,panya,nyoka.
-Mmayai hukusanywa zaidi.
-Kuku hufugwa zaidi kibiashara rahisi kulindwa magonjwa na wadudu.
-Mbolea hupatikana kwa wingi
ULEAJI BORA WA VIFARANGA
Mambo mengi yana usika katika uleaji wa vifaranga.Uleaji hutofautiana kati ya vifaranga wa kuku wa mayai na kienyeji na kuku wa nyama katika lishe na chanjo.
MATAYARISHO
- Banda liwe imara kuepuka wizi wa wanyama wasumbufu kama nyoka,paka,mwewe na kunguru.
- Banda lijengwe sehemu yenye hewa safi ya kutosha na kavu isiyo na unyevu nyevu
- Kabla ya kuingiza safisha banda nje na ndani kwa kutumia dawa yakuua vijidudu vya magonjwa.Paka chokaa kuta za ndani na hakikisha banda haliwi na joto kali,baridi kuingia,mvua na upepo mkali.
- Tayarisha chakula bora na vifaa vya kulishia na kunyweshea maji,tandiko safi na dawa.
KABLA YA KUFIKA VIFARANGA
Banda liwe tupu kwa wiki moja baada ya kusafisha kwa dawa.Vifaranga utakao pewa watoke kwenye mzalishaji mwenye historia nzuri.
- Usichanganye vifaranga wa sehemu tofauti
- Vifaranga hawawezi kuathirika haraka na mazingira hivyo ya faa kuwa na uangalifu wa hewa,mwanga na joto.
- Vifaa vya mwanga na joto ni muhimu na lazima katika kulea vifaranga.
- Tangazi za mduara kwa kutumia hard yenye urefu wa cm 60 na katikati weka balbu au jiko la mkaa na taa ya mafuta kisha mwanga wa kutosha ili vifaranga waone chakula na maji
- Weka chokaa halafu maranda tandika chilk paper au magazeti juu ya maranda.
- Masaa matano kabla ya kufika vifaranga washa joto au jiko la mkaa kwaajili ya joto liwe la nyuzi linakuwa la wastani wiki ya 1-35 nyuzi joto.
NB.Tumia maji ya mvua au ya bomba chemsha yapooze ili kuharibu chroline pia usitumie dawa ya kuua wadudu.
Siku ya tatu kabla ya chanjo usitumie ant biotic na siku tatu baada ya chanjo wasipewe antibiotic wapewe vitamin tu.
Rudia chanjo ya new castle kila baada ya mieze mi tatu chanjo ya maleks hufanyika kwa mzalisha.(Hatchery).
TIBA KWA MINYOO
Hii hufanyika kwenye kuku wa mayai mara ya kwanza hupewa wiki 8-12 na hurudiwa kila bada ya miezi mi tatu.
KUKU WA NYAMA(BROILER)
Kuku wa nyama anatakiwa apate eneo la futi moja ya mraba.Nyumba iwe na madirisha ya kutosha,hewa safi ,sakafu iwe na godoro(LITTER) ya maranda ya mbao au maganda ya mpunga.
VIFAA
Tayarisha vyombo vya chakula na maji yakutosha kulingana na idadi ya kuku.Vifaranga 100 wanaweza kutumia chombo kimoja cha kulishia(chick plate) na chombo kimoja cha kunweshea maji kwa wiki moja ya mwanzo.Wiki ya pili na kuendelea tumia feedr moja yenye kipimo chasentimita 38 kwa kuku 50 na chombo kimoja cha maji kwa kuku 60.
CHAKULA KINACHO TAKIWA.
UMRI(WIKI) AINA YA CHAKULA
0-2 CHICK STATER.
3-4 BRILER FINISHER.