AINA ZA UYOGA
- Uyoga taka
- Uyoga tegemezi
- Uyoga ufaana
- Uyoga sumu
- Mbegu
- Banda la kupandia uyoga
- Vimeng'nywa
- Mifuko ya plastiki
Mbegu za uyoga hupatikana katika maduka ya kuuza mbegu si rahisi kwa mkulima kutengeneza mbegu hizo kwani huharibika upesi huchukua mwezi mmoja kuharibika
BANDA LA KUPANDA UYOGA
Banda lakupandia uyoga linakuwa na sehemu kumi na mbili sehemu ya kupandia na sehemu ya kukuzia. Sehemu ya kupandia huwa na giza chumba chote na sehemu ya kukuzia huwa na mwanga hafifu kwani uyoga wakati unaota unahitaji carbondioxide kwa wingi na oxigyen kidogo
VIMENG'NYWE
Vimeng'nywe ni mabaki ya takataka za mazao zinatumika katika kupanda uyoga mfano , mabua ya mahindi, maranda ya mbao pamba maganda ya ndizi n.k
takataka zote za mazao zinazooza zinafaa
JINSI YA KUANDA VIMENG'NYWE
Katakata vipande vidogovidogo tayari kwa kuvianda kama shamba lako
- Kuandaa vimeng'nywe kwa njia ya kuvichemsha kwa kutumia gunia au kapu
- Kuanda vimeng'nywe kwa kuvichemsha kwa mvuke ndani ya mifuko ya plastiki
- Kuchanganya mbegu na vimeng'enywa
- kupanda kwa tabaka
- Kusiha mbegu juuya vimeng'enywa
Mifuko ya plastiki ndio shamba lako la uyoga inatumika kuweka vimeng'enywa na kupandia uyoga,unaweka vimeng'enywa na kupanda mbegu kisha unafunga juu na kutoboa vitundu vitano vitano kwa kila upande unapeleka katika chumba cha kupandia baada ya wiki moja au mbili uyoga utakua umeota hivyo utahamisha katika chumba cha kukuzia chana mfuko wako kwa kutumia kisu.
No comments:
Post a Comment