Labels

Thursday, 12 October 2017

JINSI YA KUTENGENEZA SHAMPOO



 shampoo zipo za aina nyingi inategemea virutubisho na kemikali zilizotengenezwa.kuna shampoo ambazo zina harufu nzuri .kwa mfano waweza tumia perform[harufu]kama havened lemon,jasmine,peach apples) na shampoo za virutubisho kama parachichi,karoti alovera,tango,mayai.

Mfano(i)
Kutengeneza shampoo (ambayo inatumia chemical)
zilizochanganywa harufu au perfume(vyote ni kuchanganya kwa pamoja
na kukoroga tu).

Mfano(ii)
malighafi za shampoo isiyo na virutubisho/shampoo hiyo
unaweza tengeneza kwa formula mbili
.    sulphonics Acid
.    soda ash
.    maji
.    sless
.    rangi
.    perfume
.    grycelin
.    chumvi.

JINSI YA KUTENGENEZA:
HATUA YA 1.
Kwanza tayarisha malighafi zote,ziwe juu ya meza utakayo fanyia kazi,vyombo vya kufanyia viwe visafi na kumbuka kusafisha kwa maji kila unachotumia.
Tayari vifaa vya  kufanyia kazi
  • Anza na sulphonic acid vijiko (4) vya chakula tumbukiza kwenye ndoo au mashine yako.
  • Fuatia na soda ash vijiko(2) vya chai lakini kumbuka kuchanganya na maji kidogo.
  • Koroga na mwiko au na mti baada ya mchanganyiko 
  • Tia maji lita 4 nakuanzia hapo anza kukoroga kwa muda wa dakika kumi,kisha unafuatia malighafi zifuatazo
  • Strees-robo
  • Glycerine vijiko(3) vya chakula
  • Perfume-kijiko cha chai kimoja
  • Rangi-Kijiko cha chai kimoja.
  • Chumvi kijiko cha chai kimoja
   Usiweke kitu kingine na ukumbuke chumvi ni ya mwisho kama muda umefika ikiwa nzito kama uji/shampoo yako itakua tayari.

Monday, 9 October 2017

JINSI YA KUTENGENEZA MANGO PIKO.

MANGO PICLES.










   
  • Mango picles ni (achari) au (appetizer) nzuri kwa asali ya chakula.
  • Malighafi kubwa zaidi ni embe bichi.

 MATAYARISHO.
  • Maembe ya safishwe vizuri kwa kuosha vizuri kwakutumia maji safi na maembe ya oshwe kabla hayaja menywa. 
  • Embe likatwe katwe vipande bila kugusa kokwa,Vipande ivyo viwekwe kwenye kichanja baada ya kukatwa na vianikwe juani kwa muda wa nusu saa.
  • Hifadhi embezako hizo kwenye chombo kisafi waweza acha humo kwa muda wa siku 5.
  • Kwamfano embe ulilonalo ni moja tayari viungo kama nyanya vitunguu,mafuta ya kupikia,chumvi.
KUTENGENEZA.
  • Tayarisha nyanya 1/2Kg,menya maganda na kukatakata vipande vidogo.
  • Katakata vitunguu vikubwa vi 2.
  • Chumvi vijiko viwili vya chai.
  • Kijiko kimoja cha chai kwaajili ya kuifanya mango piko yako isiharibike.
  • Maji ya limau vijiko 2 vya chai.
  • Tengeneza posti ya mchanganyiko huo.Baada ya kutayarisha(rosti)hiyo,chukua vipande vyako vya embe na kuchanganya na rosti hio.
  • Kwa rosti hii embe tumia moja lenye ujazo wa 1/4kg.
  • Weka kwenye chombo na ufunge mfuniko vizur acha kwa 3-4 siku.
  • kisha enjoy mango piko yako.

Monday, 2 October 2017

KILIMO CHA UYOGA

Uyoga ni mmea ambao hauna ukijani,uyoga ni jamiiya fungi



AINA ZA UYOGA
  1. Uyoga taka 
  2. Uyoga tegemezi
  3. Uyoga ufaana
  4. Uyoga sumu
MAHITAJI KATIKA KUPANDA UYOGA
  1. Mbegu
  2. Banda la kupandia uyoga
  3. Vimeng'nywa
  4. Mifuko ya plastiki
Mbegu
Mbegu za uyoga hupatikana katika maduka ya kuuza mbegu si rahisi kwa mkulima kutengeneza mbegu hizo kwani huharibika upesi huchukua mwezi mmoja kuharibika

BANDA LA KUPANDA UYOGA
Banda lakupandia uyoga linakuwa na sehemu  kumi na mbili sehemu ya kupandia na sehemu ya kukuzia. Sehemu ya kupandia huwa na giza chumba chote na sehemu ya kukuzia huwa na mwanga hafifu kwani  uyoga wakati unaota unahitaji carbondioxide kwa wingi na oxigyen kidogo

VIMENG'NYWE
Vimeng'nywe ni mabaki ya takataka za mazao zinatumika katika kupanda uyoga mfano , mabua ya mahindi, maranda ya mbao pamba maganda ya ndizi n.k
takataka zote za mazao zinazooza zinafaa


JINSI YA KUANDA VIMENG'NYWE
Katakata vipande vidogovidogo tayari kwa kuvianda kama shamba lako
  • Kuandaa vimeng'nywe kwa njia ya kuvichemsha kwa kutumia gunia au kapu
  • Kuanda vimeng'nywe kwa kuvichemsha kwa mvuke ndani ya mifuko ya plastiki
AINA ZA UPANDAJI
  1. Kuchanganya mbegu na vimeng'enywa
  2. kupanda kwa tabaka
  3. Kusiha mbegu juuya vimeng'enywa
MIFUKO YA PLASTIKI
Mifuko ya plastiki ndio shamba lako la uyoga inatumika kuweka vimeng'enywa na kupandia uyoga,unaweka vimeng'enywa na kupanda mbegu kisha unafunga juu na kutoboa vitundu vitano vitano kwa kila upande unapeleka katika chumba cha kupandia baada ya wiki moja au mbili uyoga utakua umeota hivyo utahamisha katika chumba cha kukuzia chana mfuko wako kwa kutumia kisu.

Saturday, 30 September 2017

UFUGAJI WA SAMAKI

Aina ya samaki wafugwao ni perege, sato ngege, magenge nk. Sababu za kufuga samaki  wa jami hizo ni ;
  1.  Huishi katika maji ya kawadia yenye joto la wastani 
  2. Huzaliana kwa wingi
  3. Hula majani ambayo hupatikana kiraisi majumbani na mashambani 
       MAHITAJI KATIKA UFUGAJI WA SAMAKI

  1. Uchaguzi wa eneo
  2. Uchimbaji wa bwawa
  3. Mbolea na majivu
  4. Uwekaji wa maji
  5. Upendaji wa vifaranga
  6. Usafishaji wa bwawa
      UCHAGUZI WA ENEO

  1. Pasiwe na mteremko mkali
  2. Pawe na udongo unaohifadhi maji
  3. Pawe na maji ya kudumu
  4. Pawe karibu na nyumbani
     UCHIMBAJI WA BWAWA
  1. Safisha eneo kisha lipime kulingana na ukubwa wa mahitaji ya bwawa lako
  2. Pima kingo weka kamba kuonyesha sehemu kingo zako zitakapopita
  3. Chonga sakafu yako chini na  sawazisha kuta zote za juu.
  4. Panda majani ya mudu ili kuzuia mmomonyoko

Friday, 29 September 2017

MALIGHAFI ZAKUTENGENEZA CHAKULA BORA CHA KUKU WA NYAMA(BROILER)

  1. MAHINDI.
  2. MASHUDU YA ALIZETI(mabaki ya alizeti baada ya kuondolewa mafuta)
  3. Mashudu ya pamba.
  4. Dagaa.
  5. Damu.
  6. Pluard.
  7. Pumba ya mashudu.
  8. Lime store.
  9. mifupa
  10. chumvi.
  11. Premix.
JINSI YA KUTENGENEZA CHAKULA CHA KUKU BORA WA NYAMA(BROILER).
  1. Mahindi-200kg-100kg.
  2. Mashudu ya alizeti-40kg-20kg.
  3. Dagaa-35kg-20kg.
  4. Damu-19kg-10kg.
  5. Pluard-65kg-35kg.
  6. Pumba ya mashudu 55kg-30kg.
  7. Lime store 25kg-20kg
  8. Mifupa 10kg-5kg.
  9. chumvi 2kg-2kg.
  10. Premix 2kg-2kg.
Waweza kuchanganya mchanganyiko huu kiasi chochote unacho weza zingatia kanuni yaani maelezo ya msingi.

GROWER MASHI
CHAKULA CHA KUKU
Mahindi    -165kg-85kg.
Pumba       -35kg-20kg
Dagaa        -35kg-50kg
pumba       -80kg-45kg
Mifupa       -7kg-5kg
Alizeti        -55kg-25kg
Chokaa       -25kg-13kg
Chumvi      -1.5kg-1.5kg
Premix      -2kg-2kg
Rice polish -85kg-45kg.

CHICK MASH BROFER,LAYER'S,KIENYEJI.
Mahindi -27kg-140kg.
Pumba   -27kg-25kg.
Mifupa  -7kg-25kg.
Alizeti    -75kg-48kg chokaa 1.5-1kg.
Chumvi  -2kg-1kg
Premix   -1kg-1kg.
Lysine    -0.6-0.3kg
Dop 1 meth 10 mine-0.6kg-0.4kg.

Friday, 22 September 2017

UFUGAJI WA KUKU.


Kuku wa kienyeji.
kujenga banda lakuku.
Unavyoanza kujenga banda la kuku kitu cha kwanza kupangilia mpangilio mzima wa mabanda yatakayo kaa:
  • Upepo.
  • Sehemu iwe inafikika
  • Na isiwe na unyevunyevu.
Mpangilio wa mabanda. 
Banda la kwanza kabisa ni banda la kuku wa nyama ndio lina jengwa mwanzoni,kuwe na upepo wa kutosha na banda linalo fuata ni kuku wa mayai,banda la mwisho kabisa ni banda la kuku wa kienyeji hili lina jumuisha bata,bata mzinga pamoja na kanga na ndege wengine wafugwao
sababu zinazo fanya ujenzi huu wa banda bora uwe wa mpangilio ni hizi zifuatazo;

(1) Magonjwa mengi ya kuku yana ambukizwa kwa njia ya hewa hivyo huwauwa zaidi kuku wa nyama wanao wahi kutoka bandani  ni rahisi kupata maambukizi kutoka kwenye kuku wanao kaa mdamrefu bandani.

(2)Kwamfano kuku wa kienyeji,bata,bata mzinga,kanga hukaa bandani mda mrefu sana hivyo magonjwa ya kuambukiza huwa wana kaanayo sana mwilini mwao kwaiyo wao wanakua wamejijengea kinga mwilini mwao tofauti na kuku wa nyama.

ULISHAJI WA KUKU WA KIENYEJI.














1)Kula kwa kuzurura(free range system)
2)kula kwa kufungwa/kwenye mabanda.

1)Njia ya kuzurura.
Kuku wanaofunguliwa tu na kuanza kutafuta chakula wenyewe njia hii ni rahisi lakini kutoa dawa kwa kulisha ni ngumu kwasababu kuku wanapo rudi jioni huwa wameshiba hivyo huwezi wapa dawa kirahisi.
2)Njia ya kufugia kwenye banda.
Njia hii ni nzuri lakini ina madhara kwa mfugaji asiye makini kwasababu inaitaji uangalizi mzuri katika kulisha chakula kwani  virutubisho vingi vya kwenye chakula kuku anaye zurura anauwezo wa kujitafutia mwenyewe nakuweka uwiano wa virutubisho ndani ya mwili wenyewe.
  KUZUIA MAGONJWA YA KUAMBUKIZWA WENYEWE KWA WENYEWE

1)MABORESHO YA UFUGAJI.
     Kwakawaida kuku wa kienyeji huchukua miezi 5-6 kuanza kutaga mayai lakini chakula bora kimefuta mfumo huo hivyo kuku wakienyeji sikuizi huchukua miezi mi 4 na kuanza kutaga,kama utafuata ufugaji bora na chakula bora hutaga mayai 100 kwa mwaka.
 MABANDA.
         Mabanda yawe na hewa ya kutosha ili waweze pumua vizuri bila kushikana.
2)Waweza weka bembea ndani ya nyumba huwafanya kuku mifupa itanuke kila wanapo ruka ni mazoezi ya kujenga mwili.
3)AINA MBILI ZA KUFUGA KUKU WA/NDANI(INTENSIVE SYSTEM)
1)Berry charge system(ufugaji wa kutumia vyuma au mbao).
2)Deep litre system.
Njia ya kulisha kuku katika banda tunatakiwa maranda,majani ya mpunga/ngano,Pumba hutumika kiasi cha 12.20 za ujazo.

FAIDA ZAKE.
-Kuku wengi hufugwa katika sehemu ndogo.
-kuku hupata kinga za hali ya hewa,jua na baridi.
 Pia hukingwa zaidi na wanyama wasumbufu kama mwewe,panya,nyoka.
-Mmayai hukusanywa zaidi.
-Kuku hufugwa zaidi kibiashara rahisi kulindwa magonjwa na wadudu.
-Mbolea hupatikana kwa wingi

ULEAJI BORA WA VIFARANGA
 Mambo mengi yana usika katika uleaji wa vifaranga.Uleaji hutofautiana kati ya vifaranga wa kuku wa mayai na kienyeji na kuku wa nyama katika lishe na chanjo.
MATAYARISHO
  •      Banda liwe imara kuepuka wizi wa wanyama wasumbufu kama nyoka,paka,mwewe na kunguru.
  •      Banda lijengwe sehemu yenye hewa safi ya kutosha na kavu isiyo na unyevu nyevu 
  •      Kabla ya kuingiza safisha banda nje na ndani kwa kutumia dawa yakuua vijidudu vya magonjwa.Paka chokaa kuta za ndani na hakikisha banda haliwi na joto kali,baridi kuingia,mvua na upepo mkali.
  • Tayarisha chakula bora na vifaa vya kulishia na kunyweshea maji,tandiko safi na dawa.

                               KABLA YA KUFIKA VIFARANGA

 Banda liwe tupu kwa wiki moja baada ya kusafisha kwa dawa.Vifaranga utakao pewa watoke kwenye mzalishaji mwenye historia nzuri.
  • Usichanganye vifaranga wa sehemu tofauti
  • Vifaranga hawawezi kuathirika haraka na mazingira hivyo ya faa kuwa na uangalifu wa hewa,mwanga na joto.
  • Vifaa vya mwanga na joto ni  muhimu na lazima katika kulea vifaranga.
  • Tangazi za mduara kwa kutumia hard yenye urefu wa cm 60 na katikati weka balbu au jiko la mkaa  na taa ya mafuta kisha mwanga wa kutosha ili vifaranga waone chakula na maji 
  • Weka chokaa halafu maranda tandika chilk paper au magazeti juu ya maranda.
  • Masaa matano kabla ya kufika vifaranga washa joto au jiko la mkaa kwaajili ya joto liwe la nyuzi linakuwa la wastani wiki ya 1-35 nyuzi joto. 
NB.Tumia maji ya mvua au ya bomba chemsha yapooze ili kuharibu chroline pia usitumie dawa ya kuua wadudu.
     Siku ya tatu kabla ya chanjo usitumie ant biotic  na siku tatu baada ya chanjo wasipewe antibiotic wapewe vitamin tu.
 Rudia chanjo ya new castle kila baada ya mieze mi tatu chanjo ya maleks hufanyika kwa mzalisha.(Hatchery).

TIBA KWA MINYOO
      Hii hufanyika kwenye kuku wa mayai mara ya  kwanza hupewa wiki 8-12 na hurudiwa kila bada ya miezi mi tatu.

KUKU WA NYAMA(BROILER)
Kuku wa nyama anatakiwa apate eneo la futi moja ya mraba.Nyumba iwe na madirisha ya kutosha,hewa safi ,sakafu iwe na godoro(LITTER) ya maranda ya mbao au maganda ya mpunga.

VIFAA
  Tayarisha vyombo vya chakula na maji yakutosha kulingana na idadi ya kuku.Vifaranga 100 wanaweza kutumia chombo kimoja cha kulishia(chick plate) na chombo kimoja cha kunweshea maji kwa wiki moja ya mwanzo.Wiki ya pili na kuendelea tumia feedr moja yenye kipimo chasentimita 38 kwa kuku 50 na chombo kimoja cha maji kwa kuku 60.

CHAKULA KINACHO TAKIWA.

UMRI(WIKI)                                                                AINA YA CHAKULA
 0-2                                                                                    CHICK STATER.
3-4                                                                                      BRILER FINISHER.

Tuesday, 2 May 2017

UEFA: Christiano Ronaldo aizamisha Atletico Madrid

Christiano Ronaldo baada ya kuiwezesha timu yake ya Real Madrid kuichapa Atletico Madrid mabao 3-0

Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Real Madrid Christiano Ronaldo amekuwa mwiba mchungu baada ya kuiwezesha timu yake ya Real Madrid kuichapa Atletico Madrid mabao 3-0 katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza uliopigwa hapo jana jumanne katika dimba la Estadio Santiago Bernabeu jijini Madrid.


Ronaldo alipachika mabao hayo katika dakika ya 10 kipindi cha kwanza na kuandika bao la pili dakika ya 73 kipindi cha pili ,huku akihitimisha karamu ya mabao matatu dakika ya 86 kipindi cha pili.

Na hii leo jumatano usiku inatarajiwa kupigwa nusu fainali nyingine kati ya Fc Monaco dhidi ya Juventus huko Stade Louis jijini Monaco.

Na wakati huo huo Mshambuliaji nyota wa Fc Monaco Radamel Falcao amesema hana mpango wowote wa kuondoka katika klabu hiyo ambayo inafukuzia mataji mawili msimu huu, la Ligue 1 na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Sunday, 30 April 2017

Mbao fc yaivua Ubingwa Yanga


Klabu ya soka ya Mbao fc ya jijini Mwanza nchini Tanzania Jana imefanikiwa kuwafunga Mabingwa wa soka Tanzania bara na Kombe la Shirikisho Tanzania klabu ya Yanga Bao 1-0 kwa bao la kujifunga kupitia kwa Vincent Andrew 'Dante' na kutinga hatua Fainali .
Hivyo kwa matokeo hayo sasa Mbao fc mwishoni mwa juma hili watakutana na Simba Sc katika hatua ya fainali.
Simba sc Klabu wao walifanikiwa kutinga fainali ya michuano hiyo kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam fc , Mshindi wa Kombe hili ndie atakayeiwakilisha Tanzania Bara katika Mashindano ya Kombe la Shirikisho kwa Msimu ujao.

Soma hapa kujua ni nafasi ngapi za kazi serikali ime tangaza.

Serikali kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia watanzania  wenye sifa na uwezo kujaza jumla ya nafasi wazi za kazi 2,748 kwa ajili ya waajiri mbalimbali Nchini.
Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi nafasi hizo za kazi ambazo zinapatikana katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz ni kwa ajili ya waajiri mbalimbali wa Ofisi za Umma.
Daudi alitaja nafasi za kazi zinazotangazwa kuwa ni Afisa Uvuvi daraja la ii, Mvuvi msaidizi daraja la ii, Afisa Mifugo msaidizi daraja la ii, Afisa mifugo daraja la ii, Mteknolijia wa samaki daraja la ii, Daktari wa mifugo daraja la ii,Afisa utafiti Mifugo daraja la ii, Daktari utafiti Mifugo daraja la ii, Fundi sanifu Maabara Mifugo daraja la ii, Mkufunzi Mifugo daraja ii, Mkufunzi wa Mifugo msaidizi na Daktari Mifugo.
Kada nyingine ni Mkufunzi daraja la ii, Mtekinolojia wa Samaki msaidizi daraja la ii, uunda boti daraja ii, nafasi 2, Dereva wa vivuko daraja la ii, msaidizi mifugo,afisa kilimo daraja la ii, Afisa kilimo msaidizi daraja la ii, Mhandisi kilimo daraja la ii, Fundi sanifu daraja la ii, Afisa utafiti kilimo daraja la ii, Mkufunzi wa kilimo msaidizi, Afisa kilimo msaidizi daraja la iii,Dereva daraja la ii, mlinzi, Mhasibu mkuu daraja ii, Msanifu lugha mkuu iii  na Afisa vipimo.

Aina ya simu za smartphone kudhibiti kisukari

Simu moja aina ya smartphone imechukuwa jukumu muhimu katika majaribio ambayo huenda yakawasaidia mamilioni ya watu duniani ambao wanakabiliwa na ugonjwa wa kisukari kuweza kuthibti kiwango cha sukari.

Watafiti wa China katika jarida la sayansi wanasema walivumbua seli za insulini na kuzidunga ndani ya panya ili kufanya kazi wakati zinapoangazwa na mwanga wa LED.
Mwanga huo ulizalishwa na programu ya simu hiyo aina ya smartphone baada ya kupokea data kutoka kwa kifaa cha kupimia damu ilio na sukari ndani ya panya huyo.
Kwa sasa watu walio na kisukari hupimwa damu ili kubaini ni wakati gani wanahitaji sindano za insulini.

Friday, 28 April 2017

Korea Kaskazini ‘yashindilia msumari’ baada ya Marekani kupeleka Meli za Kivita


Serikali ya Korea Kaskazini imetoa tamko la msimamo mkali kufuatia hatua ya Marekani 
kusogeza meli zake za kivita katika rasi ya nchi hiyo siku chache zilizopita.
Nchi hiyo imetangaza kuwa inaendelea na mpango wake wa kufanya jaribio kubwa zaidi la bomu na makombora ya nyuklia litakalokuwa la sita na kwamba hawatakoma hata kama Marekani itaendelea na mipango yake ambayo wamedai ni ya chuki.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki za Binadamu kwenye Chuo cha Jamii cha Korea Kaskazini aliyepewa mamlaka ya kuzungumzia masuala ya mgogoro wa nchi hizo mbili, Sok Chol Won jana aliiambia CNN kuwa mpango huo kabambe uko palepale.
“Majaribio ya mabomu na makombora ya nyuklia ni muhimu kwetu kama sehemu ya juhudi za kuimarisha nguvu zetu za nyuklia,” alisema.
“Wakati ambapo Marekani inaendelea na hatua zake za chuki na hasira, majaribio ya nyuklia na makombora hayatakoma,” alisisitiza.
Kauli hiyo imekuja wakati ambapo Baraza la Mawaziri la Marekani limeweka msisitizo wa kuiwekea Korea Kaskazini vikwazo vya kiuchumi na kidiplomasia huku ikitoa wito pia wa kuwepo kwa mazungumzo.
Hata hivyo, Rais Donald Trump na Makamu wake wamesisitiza uwezekano wa kuwepo hatua za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini.

Serena: Nilionyesha mimba yangu kimakosa

Serena Williams amesema kuwa alifichua kuhusu mimba yake kimakosa baada ya kuweka picha kwa Snapchat.
Serena Williams amesema kuwa alifichua kuhusu mimba yake kimakosa baada ya kuweka picha kwa Snapchat.
Bingwa huyo wa taji la Grand slam mara 23 alichapisha picha katika mtandao huo wa kijamii akijiangalia katika kioo akiwa ameandika ujumbe wiki 20 kabla ya kufuta kabla ya wasimamizi wake kuthibitisha habari hizo.
Williams mwenye umri wa miaka 35 alisema kwamba alipiga picha kila wiki ili kufuatialia mimba yake.
''Nilikuwa nikijihifadhia'', alisema.
''Nilikuwa nikiendelea vizuri lakini bahati mbaya picha moja nikaichapisha katika Snapchat''.
Bingwa huyo nambari moja kwa upande wa wanawake anatarajiwa kujifungua majira ya vuli, akisema kua aligundua kwamba ana mimba siku mbili kabla ya mashindano ya Australia Open mnamo mwezi Januari.
Williams mwenye umri wa miaka 35 alisema kwamba alipiga picha kila wiki ili kufuatialia mimba yake.


Guardiola: Sijui kama Bravo atatuchezea tena



Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema hafahamu iwapo mlindalango wa klabu hiyo Claudio Bravo ataweza kucheza tena baada ya kuumia wakati wa mechi kati ya City na Manchester United Alhamisi.
Bravio, 34, aliondolewa uwanjani kwa machela baada ya kuumia akijaribu kuondosha mpira kutoka eneo la hatari wakati wa mechi hiyo ya Ligi ya Premia.
Willy Caballero aliingia nafasi yake.
"Bila shaka ni jeraha, labda litamuweka nje wiki kadha," alisema Guardiola,
"Sijui kama ataweza kucheza tena msimu huu."
Sare hiyo tasa, ambayo Bravo aliondoka uwanjani dakika ya 79, ilikuwa mechi yake ya sita kucheza kati ya 22 alizocheza Ligi ya Premia bila kufungwa tangu anunuliwe £15.4m kutoka Barcelona.

Mourinho Sergio aguero alitumia werevu baada ya kugongwa kichwa na Marouane Fellaini.




Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema Sergio Aguero alitumia werevu baada ya kugongwa kwa kichwa na Marouane Fellaini.
Fellaini, 29, alioneshwa kadi nyekundu moja kwa moja dakika ya 84, sekunde chache baada yake kuoneshwa kadi nyingine ya manjano kwa kumtega nyota huyo wa Argentina.
Mechi hiyo ya Ligi ya Premia ilimalizika sare tasa.
"Sikutazama tukio hilo lakini naweza kufikiria kwamba labda kadi nyekundu na ilitokana na uchezaji wa uzoefu, na ujanja kiasi wa mchezaji huyo wa Argentinia," alisema Mourinho.
Alipoulizwa iwapo kiungo wa Ubelgiji Fellaini hakutumia busara, Mourinho alisema: "Marouane anasema ilikuwa kadi nyekundu kwa sababu yeye ni Marouane.
"[Mwamuzi] Martin Atkinson aliniambia kwa maoni yake ilikuwa kadi nyekundu, lakini nilimuona Aguero baadaye na hakuwa ameumia pua, hakuwa na jeraha kichwani, na uso wake ulikuwa na tabasamu kama kawaida. Sina uhakika…
"Iwapo Sergio hangejiangusha basi bila shaka haingekuwa kadi nyekundu, lakini Marouane alimpa fursa ya kufanya hivyo ….Sijui, lakini ninachokifahamu ni kwamba tulicheza dakika 15 na wachezaji 10 na vijana wetu walicheza vizuri sana, walipigania kuondoka na alama moja."
Felliani sasa amefukuzwa uwanjani mara tatu tangu ajiunge na United kutoka Everton kwa £27.5m mwezi Septemba 2013.
Awali, alifukuzwa uwanjani wakati wa mechi iliyomalizika sare tasa na Hull City mnamo 24 Mei 2015 na mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Real Sociedad mwezi Novemba 2013.
Fellaini pia alifukuzwa wakicheza mechi iliyomalizika sare 1-1 akichezea Everton dhidi ya Bolton katika Ligi ya Premia 2010.

Thursday, 27 April 2017

Man city na Mashetani wekundu man united watoka sare.






Mchezo wa dabi ya jiji la Manchester kati ya Mashetani wekundu wa Man United na Man City umemalizika kwa sare ya bila kufunga mchezo huo ulipigwa katika dimba la Etihad.
Kutoshana nguvu kwa timu hizi kunafanya vita ya kuwania nafasi nne za juu kuendelea kuwa kali City wako nafasi ya nne kwa alama 65 alama moja mbele ya United walioko nafasi ya tano kwa alaam 64.
Man city wakiwa wenyeji wa mchezo huo waliutawala mchezo kwa asilimia kubwa na umiliki wa mpira ukiwa ni asilimia 69 kwa 31.
United walibaki pungufu katika dakika ya 84 baada ya kiungo wake Marouane Fellaini kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje kwa kadi nyekundu, baada ya kumpiga kichwa Sergio Aguero.Huu ulikua ni mchezo wa 24 kwa Man united wakicheza bila kupoteza msimu huu

Wednesday, 26 April 2017

Suruali chafu zauzwa dola 425

Wengi katika mitandao ya kijamii wameishutumu kampuni hiyo ya mavazi

Kampuni moja ya mavazi nchini Marekani imeshutumiwa vikali kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutangaza kwamba inauza suruali za jeans zilizo na uchafu kwa $425 (£330; €390).
Kampuni ya Nordstrom imezipa suruali hizo jina Barracuda Straight Leg.
Suruali hizo zimebandikwa matope yaliyokauka.
Jeans hizo zimeelezwa na mtandao wa Nordstrom kuwa kiashiria cha maisha magumu ya Wamarekani wafanyakazi na pia dhihirisho la kutia bidii kazini.
Lakini wakosoaji kwenye Facebook wamesema mavazi hayo ya kampuni hiyo yanasikitisha.
"Unaweza kupata sura sawa kwa kutumia pesa kidogo sana, kwa kujigaragaza kwenye shamba lako au kwenda shambani kulima na kupalilia mimea au maua," mmoja alisema.
Mtangazaji wa kipindi cha Dirty Jobs katika runinga ya Discovery Channel Mike Rowe amesema suruali hizo "zinaonekana kama zimevaliwa na mtu aliyefanya kazi yenye uchafu mwingi" lakini "zimeshonewa watu wasiogusa uchafu".
Nordstrom imesema mavazi hayo yamepakwa matope maalum na kukaushwa na lengo ni kuonyesha kwamba anayeyavalia hana wasiwasi wa kupata uchafu akifanya kazi yoyote ile.
Nipe jeans zako kisha uniongezee dola 200, nitakuandalia vazi lako. Unaweza kuamua iwapo unataka uchafu wa kinyesi cha farasi au kuku, grisi kutoka kwenye trekta au udongo wa mfinyanzi... na kwa $600 nitampa mbuzi atafune jeans zako na kutoboa mashimo," aliandika mmoja wa wakosoaji.
Lakini kunao wengine waliosema iwapo kuna watu wanaoweza kulipa $400 kununua mavazi hayo machafu, basi nawalipe.
Mwezi jana Nordstrom walianza kuuza jeans zenye 'dirisha magotini' ambazo zinauzwa $95 (£74; €87) .

Mhalifu mtanashati zaidi azuiwa kuingia Uingereza



Jeremy Meeks, ambaye wakati mmoja alijizolea sifa za kuwa "mhalifu mtanashati zaidi duniani", amezuiwa kuingia Uingereza.
Mwanamitindo huyo alivuma sana mtandaoni mwaka 2014 picha yake ilipopakiwa kwenye mtandao.
Taarifa zinasema alijaribu kuingia Uingereza kwa shughuli za kikazi.
Maafisa wa uhamiaji walimzuia Jumanne katika uwanja wa ndege wa Heathrow, London na tayari amesafirishwa kurejeshwa Marekani.
Maafisa wa wizara ya mambo ya ndani wameambia BBC kwamba wanafahamu kuhusu kisa hicho, lakini hawawezi kuzungumzia kisa cha mtu binafsi.
Hata hivyo, kifungu 320 cha sheria za uhamiaji za Uingereza kinasema maafisa wa uhamiaji uwanja wa ndege au mpakani wanaweza kumzuia mtu yeyote ambaye amefungwa jela kati ya miezi 12 na miaka minne kuingia Uingereza.
Mtu kama huyo hata hivyo hawezi kuzuiwa miaka 10 baada yake kumaliza kutumikia kifungo.
Sheria hiyo ni miongoni mwa masharti mengine yanayoweza kutumiwa kuzuiwa watu waliofungwa jela mataifa ya nje kuingia Uingereza.

Jeremy Meeks alishtakiwa kosa la kuwa na bunduki 18 Juni 2014 na akafungwa jela hadi Machi mwaka jana.
Awali, alikuwa ametumikia kifungo cha miaka tisa kwa kosa la wizi kuanzia 2002 hadi 2011.
Jeremy amekuwa akitafutwa sana na kampuni za mitindo ya amvazi.
Meneja wa Jeremy, Jim Jordan, ameambia Daily Mail kwamba mwanamitindo huyo alikuwa amebeba stakabadhi zifaazo pamoja na barua kutoka kwa afisa wa kumfuatilia mfungwa anayetumikia kifungo cha nje.
Jeremy anadaiwa kutia saini mkataba na kampuni ya White Cross Management siku chache baada ya kuondoka jela mwaka jana.
Alishiriki maonesho ya mitindo mara ya kwanza Wiki ya Mitindo ya New York mwezi Februari.
Picha yake iliyopakiwa na polisi wa Stockton ukurasa wao wa Facebook 2014, imependwa zaidi ya mara 101,000 na kusambazwa mara 12,600.

Barca, Madrid zapeta La Liga



Miamba ya soka la Hispania vilabu vya Barcelona na Real Madrid vimendelea kutamba katika ligi hiyo kwa kupata ushindi wa mabao mengi katika michezo yao.
Barcelona waliichapa timu inayoburuza mkia katika ligi Osasuna, kwa mabao 7 -1 mabao ya Barca yakifungwa na Lionel Messi aliyefunga mabao mawili, Andre Gomes, nae akafunga mawili kinda Francisco Alcacer, akatupia nae magoli mawili huku Javier Mascherano, akifunga bao moja.

Real Madrid wakiwa ugenini katika dimba la Municipal de Riazor, waliwafunga Deportivo La Coruna, kwa mabao 6-2, mabao ya Real yalifungwa na James Rodriguez, aliyefunga mara mbili na mengine yakifungwa na Alvaro Morata, Lucas Vazquez, Isco na kiungo Casemiro
Leganes wakashinda kwa 3 - 0 dhidi ya Las Palmas, Nao Valencia wakalala nyumbani kwa kufungwa 3-2 na Real Sociedad.

Arsenal, Tottenham zashinda Epl


Mshike mshike wa kuwania ubingwa wa ligi kuu England umeendelea kushika kasi ambapo Tottenham Hotspur walipata ushindi ugenini wa bao 1-0 dhidi ya Crystal Palace.
Bao pekee la Spurs katika mchezo huo lilifungwa na kiungo Christian Eriksen, katika dakika ya 78 ya mchezo na hivyo kuendelea kuwakimbiza vinara wa ligi hiyo Chelsea, wanaongoza ligi kwa alama 78 huku Spurs wakiwa nafasi ya pili kwa alama 74.
Nao washika mititu wa London Arsenal, walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Leicester City, bao la kujifunga la beki wa Leicester Robert Huth, ndio liliwapa vijana wa Wenger alama tatu muhimu na kusogea mpaka nafasi ya sita katika msimamo wa ligi.
Vibonde wa ligi Middlesbrough wakautumia vyema uwanja wa nyumbani wa Riverside kuwa kuwachapa kwa bao 1-0 vibonde wengine wa ligi Sunderland ambao ndio wanaburuza mkia katika ligi hiyo.

Arsenal kucheza dhidi ya leicester


Arsene Wenger akiishangilia timu yake baada ya kuibandua Manchester City katika kombe la FA
Mshambuliaji wa Arsenal Alex Oxlaide Chamberlain huenda akashiriki katika mechi dhidi ya Leicester City Licha ya kuondoka katika uwanja wa Wembley baada ya mechi ya Jumapili ya FA akiuguza jeraha.
Kiungo huyo wa kati aligongwa katika mguu lakini kcha Arsene Wenger anasema kuwa alichukua hatua ya tahadhari.
Mchezaji wa Leicester Wes Morgan anauguza jereha la mguu huku msimu wa Nampalys Mendy ukikamilika baada ya kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu.
Beki Robert Huth anarudi baada ya kuhudumia marufuku ya ligi ya klabu bingwa ,lakini Slimani anaendelea kuuguza jeraha.

Wenger: Sitamuuza Sanchez kwa wapinzani wangu

Sanchez
Mshambuliaji wa Arsenal Alexi Sanchez hatouzwa kwa kilabu ya ligi ya Uingereza kulingana na mkufunzi Arsene Wenger.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kutoka Chile, ambaye alifunga bao la ushindi katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Manchester City ana mwaka mmoja uliosalia katika kandarasi yake lakini bado hajatia saini kandarasi mpya.
''Sidhani kama unaweza kumuuza kwa klabu yoyote ya Uingereza, huo ni ukweli'', alisema Arsene Wenger.
''Lakini kama nilivyosema ,nadhani atasalia na kuweka saini kandarasi mpya''.
Wenger bado hajathibitisha iwapo atasalia katika klabu hiyo ya London kaskazini, lakini anasema anafanya kazi ya kuwasajili wachezaji wapya msimu ujao.
Kandarasi ya raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 67 inakamilika mwishoni mwa msimu na amepewa kandarasi mpya.
''Nafanya kazi hadi siku ya mwisho ya msimu'', alisema Wenger mwenye umri wa miaka 67.
''Wachezaji wanaonunuliwa ndio mpango wa kila klabu katika siku zake za usoni'' ,alisema Wenger.
''Swala la iwapo nitasalia au la sio muhimu kwa sasa, kilicho muhimu ni siku za usoni za klabu hii'',Wenger alisema mnamo mwezi Februari kwamba ataamua kuhusu kandarasi mpya mnamo mwezi Machi ama Aprili na baadaye kutangaza.
''Najua nitakachofanya na hivi karibuni mutajua''.

Tuesday, 25 April 2017

United Airlines wachunguza kifo cha sungura mkubwa

Sungura wakubwa huwa na thamani.
Shirika la ndege la United Airlines linachunguza kifo cha sungura mmoja mkubwa aliyefariki alipokuwa akisafirishwa kwenye moja ya ndege za shirika hilo.
Sungura huyo kwa jina Simon, aliyekuwa na urefu wa sentimeta 90, alipatikana amefariki