Uwezo wa Makombora ya Korea Kaskazini |
Korea kaskazini inaaminika kumiliki zaidi ya silaha 1000 zenye uwezo tofauti ikiwemo kombora la maasafa marefu ambalo linaweza kuishambulia Marekani.
Mpango wa Pyongyang umeendelea katika miongo kadhaa ya hivi karibuni kutoka mizinga mikubwa katika miaka ya tisini na sabini hadi makombora ya masafa mafupi mbali na yale ya masafa marefu katika miaka 80 na 90.
Mifumo ilio na uwezo mkubwa inadaiwa kufanyiwa utafiti.
- Marekani yatishia kuiadhibu Korea Kaskazini
- Kombora la Korea Kaskazini lashindwa kupaa
- Trump: tutaidhibiti Korea Kaskazini
Hivi karibuni, Korea Kaskazini ilitangaza kwamba inaunda makombora ya masafa marefu yanayoweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine ambayo yanaweza kushambulia mataifa ya magharibi.
Taifa la Korea Kaskazini linaaminika kutengeza kombora la masafa marefu zaidi ambalo wachunguzi wamelitaja kuwa KN-08 ama Hwasong-13.
Ishara za kwanza kuhusu utengenezaji huo ulifanyika Septemba 2016 ambapo taifa hilo lilifanyia majaribio mashine mpya ya roketi ambayo baadhi ya watu wanasema inaweza kurusha kombora kutoka bara moja hadi jingine.
Idara ya ulinzi nchini Marekani Pentagon inaamini kwamba Korea Kaskazini inamiliki makombora 6 aina ya KN-08, ambalo lina uwezo wa kufika hadi Marekani.
Korea kaskazini inaaminika kutengeza toleo jipya la kombora hilo linalojulikana kama KN-14.
Haahivyo makombora hayo hayajafanyiwa majaribio.
- Korea Kaskazini: Tutaishambulia Marekani kwa nyuklia
- Korea Kaskazini: Tutafanya majaribio kila wiki
- China na Marekani waitisha suluhisho la amani Korea kaskazini
Lakini mnamo mwezi Januari 2017, kulikuwa na ishara ya jaribio, muda mfupi baada ya kiongozi Kim Jong un kudai kwamba taifa hilo lilikuwa katika awamu ya mwisho ya kutengeza kombora la masafa marefu linaloweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine.
Mpango wa kisasa wa kutengeza makombora yaa Korea Kasakzini ulianza kwa kutengeza makombora ya scud ambapo yalipitia Misri mwaka 1976.
Kufikia 1984, taifa hilo lilikuwa likitengeza makombora yake kwa jina Hwasong.
Inaaminika kuwa na makombora tofauti tofauti ya masafa mafupi ambayo yanaweza kulenga taifa jirani la Korea Kusini.
Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ya Korea umeharibika na yamekuwa yakijiandaa kukabiliana kivita.
Kombora la Hwasong 5 na Hwasong 6 ambayo pia hujulikana kama Scud B na Scud C yana uwezo wa kwenda kilomita 300 na 500 mtawalia kulingana na kituo cha Marekani kinachofanya utafiti wa kuzuia kuenea kwa nuklia.
Makombora hayo yanaweza kubeba makombora ya kemikali na nyuklia.
Silaha hizo zimejaribiwa na kupelekwa katika maeneo yanayohitajika na kombora la Hwasong-6 limeuzwa nchini Iran.
No comments:
Post a Comment