Sanchez
Mshambuliaji wa Arsenal Alexi Sanchez hatouzwa kwa kilabu ya ligi ya Uingereza kulingana na mkufunzi Arsene Wenger.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kutoka Chile, ambaye alifunga bao la ushindi katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Manchester City ana mwaka mmoja uliosalia katika kandarasi yake lakini bado hajatia saini kandarasi mpya.
''Sidhani kama unaweza kumuuza kwa klabu yoyote ya Uingereza, huo ni ukweli'', alisema Arsene Wenger.
''Lakini kama nilivyosema ,nadhani atasalia na kuweka saini kandarasi mpya''.
Wenger bado hajathibitisha iwapo atasalia katika klabu hiyo ya London kaskazini, lakini anasema anafanya kazi ya kuwasajili wachezaji wapya msimu ujao.
Kandarasi ya raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 67 inakamilika mwishoni mwa msimu na amepewa kandarasi mpya.
''Nafanya kazi hadi siku ya mwisho ya msimu'', alisema Wenger mwenye umri wa miaka 67.
''Wachezaji wanaonunuliwa ndio mpango wa kila klabu katika siku zake za usoni'' ,alisema Wenger.
''Swala la iwapo nitasalia au la sio muhimu kwa sasa, kilicho muhimu ni siku za usoni za klabu hii'',Wenger alisema mnamo mwezi Februari kwamba ataamua kuhusu kandarasi mpya mnamo mwezi Machi ama Aprili na baadaye kutangaza.
''Najua nitakachofanya na hivi karibuni mutajua''.
No comments:
Post a Comment