Labels

Tuesday 2 May 2017

UEFA: Christiano Ronaldo aizamisha Atletico Madrid

Christiano Ronaldo baada ya kuiwezesha timu yake ya Real Madrid kuichapa Atletico Madrid mabao 3-0

Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Real Madrid Christiano Ronaldo amekuwa mwiba mchungu baada ya kuiwezesha timu yake ya Real Madrid kuichapa Atletico Madrid mabao 3-0 katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza uliopigwa hapo jana jumanne katika dimba la Estadio Santiago Bernabeu jijini Madrid.


Ronaldo alipachika mabao hayo katika dakika ya 10 kipindi cha kwanza na kuandika bao la pili dakika ya 73 kipindi cha pili ,huku akihitimisha karamu ya mabao matatu dakika ya 86 kipindi cha pili.

Na hii leo jumatano usiku inatarajiwa kupigwa nusu fainali nyingine kati ya Fc Monaco dhidi ya Juventus huko Stade Louis jijini Monaco.

Na wakati huo huo Mshambuliaji nyota wa Fc Monaco Radamel Falcao amesema hana mpango wowote wa kuondoka katika klabu hiyo ambayo inafukuzia mataji mawili msimu huu, la Ligue 1 na Ligi ya Mabingwa Ulaya.