Labels

Monday 21 November 2016

Wasifu wa Trump, mshindi wa urais Marekani

Donald Trump, rais mteule wa Marekani ambaye anatarajiwa kuapishwa tarehe 20 Januari mwaka 2017, ni tajiri anayemiliki majumba mengi na ambaye amekuwa mtangazaji wa kipindi cha maisha ya uhalisia kwenye runinga.
Amekuwa mtu anayeangazia sana ushindi katika maisha yake na alikuwa tangu mwanzo amesema ni lazima afanikiwe katika kupata tuzo kuu duniani, kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani.
Kwa wafuasi wake, ndiye anayeweza kuleta ufanisi kwa Marekani.
Kwao, huyu ni tajiri shupavu anayeweza kusuluhisha matatizo yote ya nchi ambayo wanahisi yameshusha hadhi ya Marekani duniani.
Wengi wao ni raia wa Marekani wafanyikazi hasa wenye asili ya Kizungu na walio na maisha ya kadri.
Mbaguzi na mfitini
Hata hivyo kwa wakosoaji wake, walisema huyu ni mbaguzi na mfitini, mfidhuli mkubwa ambaye angepokeza ushindi kwa Hillary Clinton au kuitumbukiza dunia kwenye janga kubwa. Walinoa kwa hilo la kwanza kwani alimshinda Bi Clinton kwa urahisi katika uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Novemba.

Obama: Sitanyamaza wakati wa utawala wa Trump

Bw Obama na Bw Trump walikutana White House siku mbili baada ya uchaguzi
Rais wa Marekani anayeondoka Barack Obama amesema huenda akazungumza, kinyume na utamaduni wa siasa Marekani, iwapo mrithi wake Donald Trump atatishia "maadili muhimu" ya Marekani.
Huwa desturi kwamba marais wa zamani wa Marekani huwa hawajiingizi sana katika siasa baada ya kuondoka madarakani na huwa hawazungumzi kuhusu warithi wao.
Akiongea katika kikao na wanahabari wakati wa mkutano wa nchi za Asia na Pasifiki (Apec) mjini Lima, Peru, Bw Obama amesema anakusudia kumsaidia Bw Obama na kumpa muda wa kueleza maono yake.
Lakini amesema kwamba, kama raia, huenda akalazimika kuzungumza kuhusu baadhi ya mambo.

Wednesday 2 November 2016

Thursday 27 October 2016


Njia salama ya kuongeza Makalio kwa njia salama ya mazoezi.

Miaka ya hivi karibuni kua na makalio makubwa imekua ni fasheni muhimu sana kiasi kwamba wanawake wasio na makalio makubwa wamejikuta wakipata tabu na hata kufanya upasuaji hatari ili kuongeza makalio na wengi wameharibika kabisa au kupoteza maisha kwenye oparesheni hizo hatari.
Lakini kama jinsi wanaume wanavyobeba vyuma na kuongeza vifua na mikono hivyohivyo wanawake wanaweza kuongeza misuli hiyo muhimu ya makalio ambayo kitaalamu inaitwa gluteal maximus,gluteal minimus na gluteal medias. hiyo ndio misuli mikuu mitatu ambayo kwa pamoja inaitwa makalio na ikifanyiwa mazoezi vizuri huongezeka na kua mikubwa.
Ni kweli ukubwa wa makalio na kiungo chochote cha mwili hufuata ukoo lakini pia mazoezi husaidia sana kukuza makalio au kiungo chochote cha mwili chenye misuli lakini sio kua makubwa tu lakini hata kuyafanya kua na shepu nzuri na kuvutia..

Unaweza kua hujaamini bado lakini kwa kukuthibitishia habari hizi ni kwamba jeniffer lopez mwanamuziki na muigizaji wa filamu nchini marekani ambaye anaongoza kwa kua na makalio makubwa zaidi kuliko wasanii wote mpaka akayakatia bima yaani insurance anafanya mazoezi haya kama ifuatavyo..
Mazoezi ya squat; mazoezi haya huanzwa kwa kusimama na miguu yote miwili kisha kuanza kama unakaa hewani halafu unainuka, mazoezi haya huvuta misuli ya makalio na kuibana kisha kuongeza upana na siku za kwanza za mazoezi haya mtu hujisikia maumivu na kuanza kuhisi nguo zimeanza kubana mpaka mapajani. ni zoezi kuu na muhimu katika kukuza makalio.fanya zoezi hili kwa raundi tatu kila raundi fanya mara kumi na tano au unaweza ukaanza kama picha inavyoonyesha hapo kwa mwezi mmoja kisha ukaendelea na mazoezi ya kawaida kama nilivyoelekeza.
zoezi la bridge; watu wengi wanashinda wamekaa kwenye viti  mashuleni au maofisini muda mwingi na hali hii hufanya hata mtu mwenye makalio makubwa ya kuzaliwa nayo kuanza kupoteza shepu yake nzuri ya mwanzoni. zoezi hili huanza kwa kulala chini kwa mgongo kisha inua kiuno kwa juu, sasa bakia kwa hali hii kwa muda kisha nyoosha mguu mmoja kwa mbele kwa sekunde kadhaa afu rudisha chini halafu badilisha mguu.fanya hivi kwa kila mguu mara kumi kwa raundi tatu huku ukipumzika dakika mbili kila baada ya raundi.
donkey kick; piga magoti kisha weka mikono chini kama mbuzi anavyosimama kisha inua mguu mmoja wa nyuma mpaka uangalie juu kisha rudisha chini taratibu.fanya hivi raundi tatu huku kila mguu ukiinua na kuurudisha mara 20.
kula protini nyingi: vyakula vya protini ni muhimu kujenga misuli na mifupa hivo kula sana maharage, nyama, samaki,maziwa, karanga, korosho na kadhalika. hii itakujenga haraka sana na kukupa matokeo mazuri kwani mwili unajengwa na chakula.
chagua aina nzuri ya wanga; ulaji wa mikaango kama chips, chapati, maandazi na kadhalika sio wanga nzuri kwani huleta vitambi na kukufanya ue na shepu mbaya ni vizuri kula wanga asili kama ugali,viazi,mihogo,wali na kadhalika.
tumia mboga za majani; mboga za majani ni muhimu sana kwani husaidia chakula ulichokula kiweze kunyonywa na mwili kirahisi na kupunguza uwezekanao wa kupata kitambi.
tumia virutubisho vya kutosha; virutubisho vyenye madini mbalimbali na protini ni muhimu sana kwani vyenyewe vinaenda moja kwa moja kufanya kazi kwenye mwili na kuanza kujenga misuli hii bila kuanza kufyonzwa taratibu tumboni kama vyakula vingine. utafiti unaonyesha wanaotumia virutubsho hivi hufanikiwa sana kuliko wasiotumia kabisa.jinsi ya kutumia; chota kijiko kimoja kilichowekwa kwenye virutubisho vyako kisha changanya na maziwa kwa upande wa protein shake na kwa upande wa argi changanya kijiko kimoja cha unga na maziwa ya mgando au juice.kunywa mara moja au mbili kwa siku huku ukiendelea na mazoezi.
mwisho: kama ilivyokua kwa mazoezi mengine yeyote itakuchukua muda angalau wiki mbili au mwezi mmoja kuanza kuona matokeo na haimaanishi kwamba ndio matokeo mazuri yakipatikana ndio unaacha hapana, mazoezi ni muhimu kwa mwili wa binadamu, unaweza ukaanza na zoezi la mwezi yaani mara moja kwa siku kisha endelea na zoezi hili mara tano kwa wiki baada ya mwezi wa kwanza. kumbuka kama ilivyo kwa mazoezi mengine ya mwili, unahitaji moyo wa mazoezi kufanikiwa, usije ukafanya zoezi siku mbili ukaacha afu ukategemea mabadiliko..unaweza ukatutafuta kupata virutubisho hivyo, kupata video za mazoezi na kwa msaada wa kitaalamu zaidi.

Mazoezi ya kujenga misuli ya mwili bila kunyanyua vyuma vizito.

Tofauti na unyayuaji vyuma vizito, zipo njia nyingine za kukuza misuli na kufanya mwili kuwa katika hali ya mvuto kuliko hata ya myanyua vyuma, na kuufanya mwili kujijenga kwa usawa bila kuwa na utofauti wa ukubwa wa misuli ambao wanyanyua vyuma vizito wengi wao walivyo, haya hapa ni mazoezi kumi na matano yatakayokuweka vizuri kiafya na kimuonekano...

  • Push up
  Ni zoezi linalopanua kifua, kujenga kifua, kukuza misuli ya mikono ya ndani na nje na ni zoezi zuri la kuanzia, kama unataka kuwa na mwili wa kujijenga vizuri anza na hili zoezi.

  • Pull ups
 Pull ups inafanyisha kazi kila misuli mwilini, hasa misuli ya mikono na mgongo, ukitaka uwe na nundu za mikono kama za Jean Claud Vandame hili ndo hasa zoezi lako.
  • Plank
Ukishikilia hili zoezi bila kutingishika kwa dakika kadhaa, wewe kweli utakua una nia na kuubadilisha mwili wako liwe hekalu la mvuto. Zoezi hili linahitaji mabega yaliyoshiba na linafanyisha kazi misuli ya mikono, kiuno, mgongo, shingo na miguu na zoezi hili lina zawadi moja, linafanya tumbo lako likatike mara sita.
  • Roll Out
    Hili zoezi linafanana na la nusu push up(Plank), ila linachobadilisha ni kusukuma nondo kuelekea mbele na kurudi, na jinsi unavyoendelea kusukuma nondo ndo ambavyo zoezi linavyozidi kuwa gumu, kwa hio unahitaji nia na kujitoa kweli, faida zake linajenga misuli ya mgongo, kiuno, kifua na kutanua mabega.
  • Glute bridge
    Zoezi hili linajenga mgongo na misuli yote inaouzunguka, ukiwa mkufunzi wa hili zoezi kinachofuata ni kuombwa namba tu na wasichana.
  • Iverted Row
    Hili zoezi ni la mgongo, fuata kama picha inavyolionyesha, faida zake linafanya kifua kiwe kipana zaidi na mikono iwe na stamina zaidi.
  • Close Hands Push ups
    Hili zoezi ni kwa ajili ya mikono, na ni kwa ajili ya nundu za ndani na nje ya mikono, na misuli yako inakua inakua kwa pamoja bila kutegeana, fanya hili zoezi na utaona mabadiliko makubwa kwenye mikono yako.
  • Star Plack
    Hili zoezi kidogo ni zito kidogo, na zoezi hili linalenga kifua na mabega pamoja na misuli ya miguu na mikono, na ni zuri kwa kukata tumbo.
  • Burpee
    Zoezi la kupunguza mafuta mwilini, zoezi hili linafanya mwili mzima uchemke kwa pamoja, ukiwa unafanya hili, unakua unafanyisha kazi kila kiungo cha mwili na kuondoa sehemu dhaifu mwilini.
  • Dip
    Zoezi la misuli ya nyuma ya mkono na linasaidia pia kwenye misui ya kifua na upanuaji wa mabega na kufanya kifua kikae vizuri, zoezi hili linahitaji nia na nguvu ili lifanyike kwa mpangilio unaotakiwa na linamzidi yule aliyelala kwenye benchi akinyanyua vyuma vizito.
  • Bulgaria Split Squart
    Kichura chura cha mguu mmoja nyuma, kinafanyisha kazi misuli ya mapajani na kukufanya uwe na stamina zaidi, ukifanya hili kwa wiki kadhaa, kama kichura chura cha kawaida kilikua kinakupiga chenga basi utakua unafanya mara mbili ya zaidi ulivyokua unafanya.
  • Suspended Push ups
     
    Push ups ni nzuri, ila ukiiongezea ugumu kidogo kwa kuiongezea suspenda, ni njia mojawapo ya kuiongezea misuli uzito, na kufanya iwe misuli yenye ujazo na ya muda mrefu tofauti na yule anaebeba vyuma vizito.
  • Prone Back Extension
    Hili zoezi linahimalisha kiuno, tumbo na mgongo kwa ujumla.
  • Pike Push ups
    Ukiwa mkongwe wa push ups, hili ndilo zoezi la mwisho la push ups na linasaidia kuimalisha mabega na kuongeza ubora wa viazi vyako vya mikono.
  • Swiss Ball Rollout
    Zoezi linavyozidi kuwa gumu ndo misuli inavyozidi kuongezeka, ukiweza kuzingatia haya mazoezi utajishangaa baada ya wiki tatu mfululizo ukiwa unayafanya.

Wednesday 26 October 2016

Kuwa Tajiri kwa Mtaji wa Laki 3 tu, Kupitia Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji

LEO TUANGALIE MCHANGANUO WA TSHS 300,000/= (LAKI TATU) KWA KUANZISHA MRADI WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI.
Hapa tuta hitaji kuku 11 tu wakubwa wanao taga yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku hao 11 baada ya miezi mitatu unaweza ukawa na kuku mia Tatu 300 au na zaidi kama unataka.
Nunua kuku wako katika chanzo cha kuaminika kuepuka magonjwa usinunue kuku sehemu za masokoni au kwenye mabanda ya njiani au kuku wanao safirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.
Unapo nunua kuku wakubwa kwanza unapo wafikisha wape chanjo ya mdondo (Newcastle vaccine) ili kuweka rekodi yako ya chanjo maana chanjo hii hurudiwa kila baada ya miezi 3. Ukumbuke tarehe uliyo wachanja na tarehe utakayo wachanja tena baadae.
Usinunue kuku kabla hujaandaa banda na Chakula.
Katika sh. 300000 toa sh.69500 ambayo utanunua Chakula cha kuku, kuku hawa hawana formula ya Chakula hivyo unaweza kununua material ukachanganya Chakula mwenyewe ampapo utaokoa pesa nyingi pia.
Mchanganuo Wa 69500 ni:-
Pumba gunia 1. Shs.20000 gunia la pumba lina kilo 70.
Paraza kilo 25 = 700x25 =17500. Paraza ni mahindi yaliyo vunjwa vunjwa kwaajili ya Chakula cha kuku.
Mashudu ya alizeti kilo 15. 700x15=10500
layer's consetraite
Kilo 25 kifuko. = 21500.
Ukijumlisha utakuwa umepata kilo 135 kwa shs 69500. Ambapo kila kilo moja ya Chakula utakuwa umenunua kwa shiling 514.8.
Chakula hicho kichanganye kwa kutumia chepe kichanganye vizuri kichanganyike pumba lazima iwe kavu kabisa ikaushe usiwape kuku pumba mbichi.
Kumbuka kuku anayetaga anakula Gram 130 kwa siku
Hivyo kuku 10 watakula kilo 1.3 kwa siku ambayo ni gram 1300.
Hivyo tutaweza kuona Chakula chetu kitatupeleka zaidi ya siku 100 ya zaidi ya miezi mitatu.
TOA SHS 170000 AMBAYO UTANUNULIA KUKU.
Mchanganuo wake Kwa kila kuku mzuri ambaye ajazeeka anayetaga utampata kwa shilingi 15000 na Jogoo nzuri utampata kwa shilingi 20000.
Jogoo 1 = 20000
Majike 10 x15000= 150000 jumla 170000.
Itakuwa imebaki shs. 60500
-Hii pesa iliyobaki ni kwa ajili ya kununu material ya bei nafuu na kutengeneza banda la kuku 10 hadi 20. Kuku hawa hawaitaji banda Kubwa kwasababu hawashindi ndani wataingia ndani wakati Wa kulala jiaoni na mchana wakati wakutaga Kuku wachiwe eneo la kutosha na lenye mchanga watakao itumia kuoga kuondoa wadudu km papasi na utitiri sehemu wanayopenda kuoga nyunyizia Dawa ya utitiri.
Banda tengeneza la kuhamisha la futi 4x8x4 yani urefu kwenda juu futi 4 upana futi 8 kipenyo futi 4. Tumia materio yaliyo karibu nawe kama mirunda, mabanzi, Mabati reject au yaliyochakaa chicken wire au wire mesh, fito mbao 2x2 au 4x2 n.k. Kama ni sehemu za mjini litakugharimu kama Tsh 50,000-60,000.Vijijini au nje ya mji ambapo miti ni mingi litakugharimu Tsh 25,000 hadi 35,000.
Haya jinsi ya kuwaendeleza hao kuku ili kupata kuku wengi hadi utakao wataka. Hapa itabidi ukubali kupeleka Mayai sehemu ambapo wanatotolesha ambapo trey 1 ni shilingi 10000.
Hapa kuku hawa 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku ambapo kwa mwezi ni Mayai 240. Kila baada ya siku 7 peleka Mayai kwenye Mashine yakutotolea (incubator). Hivyo kwa mwezi utapeleka Mayai 240 utapata wastani Wa Vifaranga 200. Hivyo baada ya mwezi nakushauri usitotoleshe tena hao Vifaranga 200 ni wengi sana kwa kuanzia kwa kuwa tayari tunenunua Chakula cha kuku cha kutupeleka miezi mitatu basi Mayai utakayo endelea kuokota utayauza kwaajili ya kupata hela ya Chakula cha Vifaranga watakao toka hao zaidi ya 200. Hivyo mradi huu utakuwa unajiendesha wenyewe.
Nikiwa na maana kama kuku 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku na Mayai 240 kwa mwezi ni wazi kwamba kuku hao wanakuingizia 120000 kwa mwezi ambaya sasa hela Hii itatumika kununua Chakula cha kulea hao Vifaranga ambapo Mayai ya mwezi tu yataweza kununua Chakula ambacho Vifaranga 200 watakula mwezi pamoja na chanjo na Dawa zote.
Hivyo baada ya miezi mitatu utakuwa na Vifaranga wakubwa Wa miezi miwili na Chakula cha kuku wakubwa ndo kitakuwa kinaishia hapa utachanganya Chakula cha aina moja tu wale Vifaranga watakuwa wameshakuwa kiasi cha kula Chakula chochote.

Mtu aliyevalia kama mti akamatwa Marekani

Tree guy

Mwanamume mmoja nchini Marekani, ambaye ameanza kufahamika kama "binadamu mti", alikamatwa baada yake kuvuka barabara akiwa amevalia kama mti.

Asher Woodworth, kutoka jimbo la Maine nchini Marekani, alijifunika kwa matawi na kuvuka barabara polepole.
Polisi walimsindikiza hadi kando mwa barabara kabla ya kumuweka kizuizini.
Asher baadaye aliachiliwa huru na polisi.
Aliambia BBC kwamba alikuwa akivuka barabara mara ya tatu pale alipokabiliwa na maafisa wa polisi.
Yeye ni mwigizaji mjini Portland, Maine.
Anasema: "Nilipata wazo hili nilipokuwa natafakari sana siku moja."
Anasema alikuwa anataka tu kuwashangaza watu kwa mavazi yake na kuwafanya "watafakari upya kuhusu matarajio yao".
Alikuwa ametumia matawi ya miti ya aina mbalimbali na anasema ilimchukua yeye na rafiki yake saa kadha kukamilisha vazi hilo.


Matawi
Alikuwa amepakia picha yenye vazi jingine linalokaribiana na hilo kwenye mtandao wa Tumblr mwezi uliopita 

  •  Anasema matawi ya miti aliyokuwa amevalia yalikuwa "yananukia".
  • Lakini mbona akaamua kuvalia matawi ya miti?
  • "Huwa nahisi nina uhusiano wa karibu na miti, naipenda sana," aliambia.
  • Alikuwa pia ametiwa moyo na mpiga picha Charles Freger, aliyepiga picha hii iliyo hapa chini
  •  
    Mwanamume aliyefunikwa kwa matawi
    Image caption Asher Woodworth pia aliweka picha hii ukurasa wake wa Tumblr
Baada yake kukamatwa, Asher Woodworth anasema alikaa saa sita kizuizini kabla ya kuachiliwa huru Jumatatu.

Guradiola: Nasubiri msamaha kutoka kwa Yaya Toure


Pep Guardiola na Yaya Toure
Pep Guardiola na Yaya Toure











Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anamuhitaji kiungo wa kati Yaya Toure lakini bado anasubiri kuombwa msamaha na ajenti wa mchezaji huyo.
Raia huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 33,amecheza mara moja msimu huu,katika kombe la vilabu bingwa .
Baadaye aliwachwa nje katika kinyang'anyiro hicho.Dimitri Seluk alidai kuwa Toure amefedheheshwa na uamuzi huo.
Alipoulizwa iwapo Toure angecheza katika kombe la ligi katika uwanja wa Old Trafford ,Guardiola alisema: Unajua hali ilivyo.
Raia huyo wa Uhaspania alisema mnamo mwezi Septemba kwamba Seluk lazima aombe msamaha,iwapo Toure anahitaji kucheza katika kikosi cha kwanza ,lakini ajenti huyo aliambia BBC Sport wakati huo kwamba: Ni nini ninachofaa kukiombea msamaha?Anafaa kuongea na Yaya anayemfamnyia kazi yake''.
Na huku kukiwa hakuna msamaha uliotolewa ,hakuna mapatano kati ya mkufunzi huyo na mchezaji wake.


Juan Mata alifunga bao lake la tatu msimu huu 

 Man Utd wawaondoa Man City kombe la EFL

Manchester United walifika hatua ya robo fainali katika Kombe la EFL baada ya kuwalaza mabingwa watetezi Manchester City kwenye debi iliyochezewa uwanja wa Old Trafford.

Juan Mata alifunga bao la pekee mechi hiyo baada ya kupata mpira kutoka kwa mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic.
Paul Pogba alikuwa amegonga mlingoti kwa kombora kali awali na kusisimua mechi hiyo kipindi cha pili.
Kipindi cha kwanza kilikuwa kikavu bila upande wowote kupata kombora la kulenga goli.
Manchester United sasa watakutana na West Ham ambao waliwalaza Chelsea 2-1.
Ushindi huo wa United ulikuwa wao wa pili katika mechi tano, na wa nne kwa Jose Mourinho katika mechi 18 alizokutana na Pep Guardiola.

Juan Mata
Image caption Mata walianza vyema kipindi cha pili

 


 

Justin Timberlake nusura ajipate taabani kwa sababu ya selfie

Justin Timberlake

Mwanamuziki mashuhuri nchini Marekani Justin Timberlake nusura ajipate taabani  baada yake kupakia picha yake ya kujipiga kwenye mtandao wa Instagram.
Alikuwa amejipiga picha hiyo akipiga kura yake katika mji wa Memphis, Tennessee.
Yeye ni miongoni mwa mamilioni ya wapiga kura ambao wamekuwa wakipiga kura zao mapema.
Nyota huyo wa pop, ambaye pia ni mwigizaji, hakuwa anakumbuka kwamba jimbo la Tennessee lilipiga marufuku upigaji wa picha katika vitu vya kupigia kura mwaka jana.
Afisi ya mwanasheria mkuu wa eneo la Shelby ilikuwa awali imesema "imefahamishwa kuhusu uwezekano wa uvunjaji wa sheria za uchaguzi" na kwamba kisa hicho kilikuwa kinachunguzwa.
Lakini baadaye, mwanasheria huyo Amy Weirich alisema taarifa hiyo ya awali "haikuwa sahihi" na lilitolewa kwa umma bila yeye kufahamu.
"Niko nje ya mji kwa sasa nikihudhuria kongamano. Hakuna yeyote katika afisi yetu anayechunguza kisa hiki kwa sasa. Hatutatumia rasilimali zetu adimu kufuatilia suala hili," alisema Bi Weirich.
Timberlake ana wafuasi 37 milioni kwenye Instagram.
Iwapo angefunguliwa mashtaka ya kukiuka sheria za uchaguzi, angehukumiwa kufungwa jela siku 30 au kupigwa faini $50 (£41), au apewe adhabu zote mbili.
Adam Ghassemi, msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Tennessee, amesema watu wanafaa kutumia simu zao kujisaidia katika kupiga kura pekee.


Justin Timberlake

Ni kinyume cha sheria kupiga picha katika chumba cha kupigia kura katika majimbo 18 nchini Marekani kwa mujibu wa shirika la habari la AP.
Hata hivyo, katika majimbo 20 inakubaliwa.
Jumatatu, jaji mmoja wa mahakama ya dola aliunga mkono msimamo wa mwanamume mmoja kutoka Michigan kwamba sheria inayowazuia watu kupiga picha kura zao ambazo tayari wamezijaza na kuzisambaza picha hizo mitandaoni ni ukiukaji wa haki ya kikatiba ya kujieleza.
Jumatatu, wapiga kura wengine wawili jimbo la Colorado waliwasilisha kesi kortini kupinga sheria inayozuia watu kuonyesha karatasi za kura ambazo wamezijaza kwa watu wengine. Wanasema marufuku hiyo inakiuka katiba.
Daniel Sturridge
Daniel Sturridge sasa amefunga mabao tisa katika mechi nane za karibuni zaidi alizocheza Kombe la Ligi

EFL: Sturridge asaidia Liverpool kulaza Tottenham Hotspur

 Mshambuliaji Daniel Sturridge alifunga mabao mawili na kuwawezesha Liverpool kufika hatua ya robofainali Kombe la EFL kwa kulaza Tottenham 2-1 uwanjani Anfield

Liverpool sasa wameenda mechi 10 bila kushindwa.
Sturridge aliwekwa benchi Jumamosi mechi waliyolaza West Brom na hakutumiwa.
Hata hivyo alihitaji dakika 10 pekee kufunga dhidi ya Spurs.
Jurgen Klopp alikuwa amebadilisha kikosi chache kizima kilichoanza mechi hiyo ya wikendi, Mauricio Pochettino naye akabadilisha wachezaji 10.
Spurs, walioanza na wachezaji wanane wa miaka 23 kwenda chini, walicheza vyema lakini walitatizika kushambulia hadi pale walipopata penalti iliyofungwa na Vincent Janssen baada ya nguvu mpya Erik Lamela kuchezewa visivyo eneo la hatari.
Sturridge aliongezea Liverpool bao la pili dakika ya 64.


Matokeo ya mechi za EFL

  • Arsenal 2-0 Reading
  • Bristol City 1-2 Hull
  • Leeds 2-2 Norwich
  • (Leeds United wakashinda 3-2 kupitia penalti)
  • Liverpool 2-1 Tottenham
  • Newcastle 6-0 Preston


Top five freakest body builders ever

(Orodha tano ya watunisha misuli wa kutisha duniani)


Tuesday 25 October 2016

Interview ya Diamond platnumz ndani ya BBC Africa.


Sababu ilio mfanya Jastin biber atupe mike na kushuka stejini alipokua aki akifanya shoo.

Staa wa muziki wa RnB na Pop mwenye asili ya CanadaJustin Bieber amezikamata headlines baada ya kutupa mic chini akiwa anaperfom kwenye stage za show ya Manchester usiku wa Oct 23 2016na kuondoka jukwaani hapo.
Imetajwa na kituo kikubwa cha habari cha Enewscha Marekani kuwa mashabiki kwenye show hiyo walikuwa wakipiga kelele za shangwe kupita kiasi na kumkera staa huyo ambapo alidai kuwa anataka aongee nao badala yake zinasikika kelele ndipo akamua kuchukua uwamuzi huo.
Enews waliongezea kuwa Justin alishawaonya mara ya kwanza mashabiki wasipige kelele wakati anaongea nao lakini hawakusikia na haya ndiyo yalikuwa maneno ya Justin…..

>>>’Nashukuru sana kwa upendo wenu mnao uonyesha kwangu, hizi kelele tafadhali naomba ziachwe ninashukuru tena lakini sidhani kama ni lazima kwenu kushangilia wakati naongea kwasababu najisikia kama nataka kuunganishwa na ninyi’  –Justin Bieber 


ALIYEKUWA MCHEZAJI MASHURI WA BRAZIL CARLOS ALBERTO AFARIKI AKIWA NA UMRI WA MIAKA 72


Carlos Alberto
Image captionCarlos Alberto

Aliyekuwa mchezaji mashuhuri wa timu ya Brazil Carlos Alberto ,ambaye alikuwa nahodha wa kikosi kilichoshinda kombe la dunia mwaka 1970 amefariki akiwa na umri wa mika 72.
Alifunga mojawapo ya mabao mazuri zaidi duniani katika historia ya kombe la dunia katika mechi ya fainali dhidi ya Italy mwaka 1970,baada ya kuwachenga mabeki na kufunga kupitia mkwaju mkali.
Beki wa kulia Alberto alichezeshwa mara 53 na Brazil na kushinda mataji ya nyumbani dhidi ya Fluminense na Santos ambapo alishiriki mara 400.

Alifariki mjini Rio de Janeiro kufuatia mshtuko wa moyo.



Mashindano ya urembo ya albino kufanyika Kenya


Akina dada walioshiriki katika mashindano ya urembo kwa watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi ama Albinos jijini Nairobi, Kenya. Tarehe 21 Oktoba 2016.Mfalme! Jairus Ongetta, ambaye amekabidhiwa tuzo ya uanamitindo bora kwa wanaume akiwa jukwaani na mavazi ya kupendeza. Amekuwa mwanamke wa kwanza kushinda taji hilo, katika mashindano yaliyofanyika jijini Nairobi, Kenya tarehe 21 Oktoba 2016


  • Oktoba 2016
Kuwa mlemavu wa ngozi au albino barani Afrika mara nyingi imekuwa ikihusishwa na imani potofu ikiwemo ya ushirikina na kufanya albino wengi kukabiliwa na unyanyapaa na kutengwa na jamii zao.
Kwa sasa vijana wa jamii ya albino huko nchini Kenya wamejikusanya wakijiandaa na onyesho la Miss na Mr Albino litakalofanyika hii Ijumaa.
Onyesho hilo lina lengo la kuwatia moyo watu wenye ulemavu wa ngozi na pia kubadili mtazamo wa jamii kuwa albino ni watu kama wengine.
Dayo Yusuf alitembelea kambi ya wana mitindo hao wakati walipokuwa katika maandalizi ya mwisho mwisho kuelekea kwenye onyesho hilo na kutuandalia taarifa hii ifuatayo .








Wenger: Tuna fursa nzuri ya kushinda ligi

  Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger 

Image caption Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger


Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa ana fursa nzuri ya kushinda ligi ya Uingereza msimu huu kwa mara ya kwanza tangu washinde taji hilo bila kushindwa mwaka 2004.
Akizungumza katika mkutano wa kila mwaka wa klabu hiyo,Wenger mwenye umri wa miaka 67,alisema kuwa mshindi wa taji la ligi kuu atakuwa na kati ya pointi 82 na 86 mwaka huu.
Alisema: Hii leo tuko katika nafasi nzuri zaidi ya kuwania taji la ligi ya Uingereza ikilinganishwa na miaka mitano au sita iliopita.
Ninaamini tuna timu nzuri katika ligi yenye ushindani mkubwa.
Arsenal ni wa pili katika jedwali la ligi,ikiwa ni mojwapo ya timu tatu zenye pointi 20 na wako katika nafasi ya pili kutokana na tofauti ya mabao.
Wenger anasema kuwa anafikiri kwamba anahitaji pointi 62 kutoka kwa mechi 29 zilizosalia kushinda taji .
Leicester ndio mabingwa wa taji hilo msimu uliopita.
''Baada ya mechi 9 ,tuna pointi 20,ikimaanisha kwamba ubingwa huo utaamuliwa na kati ya pointi 82 na 86'',alisema.

Samsung company explain's why galaxy note 7 battery explode


BETRI ZINAZO TUMIWA KATIKA SIMU ZINA SUMU(HASA AMBAZO NI FULL BATTERY.

Utafiti: Betri zinazotumiwa katika simu zina sumu

  • 24 Oktoba 2016
Image copyright AFP
Image caption Betri za Lithium-ion zinazodaiwa kuwa na sumu
Zaidi ya gesi 100 zinazoweza kusababisha kifo hutolewa na betri zinazopatikana miongoni mwa mabilioni ya vifaa vinavyotumiwa na raia wengi duniani kama vile simu aina ya smartphone na vipatakilishi kulingana na utafiti mpya.
Utafiti huo ulibaini gesi 100 zenye sumu zinazotolewa na betri za Lithium, ikiwemo ile ya kaboni monoksaidi, ambayo inaweza kusababisha kujikuna katika ngozi, macho na pua mbali na kuathiri mazingira.
Watafiti kutoka taasisi ya ulinzi ya NBC nchini Marekani pamoja na chuo kikuu cha Tsinghua nchini China wamesema kuwa watu wengi huenda hawajui hatari ya betri kupata moto, kuharibika ama kutumia chaji isiofaa katika vifaa hivyo, jarida la Science Explorer limeripoti.
Katika utafiti huo mpya,walichunguza betri moja ya kuchaji inayojulikana kama Lithium-ion,ambayo huwekwa katika vifaa vinavyotumika kila mwaka.
''Siku hizi,Betri za Lithium-ion hukuzwa na serikali nyingi duniani kama kawi inayopatikana kwa haraka ili kuviwasha vifaa vyote ikiwemo magari ya kielektroniki hadi simu," alisema Jie Sun, profesa mkuu katika taasisi ya ulinzi ya NBC.
Sun na wenzake waligundua sababu kadhaa ambazo zinaweza kuongeza gesi zenye sumu zinazotolewa.
Betri zilizopata chaji zaidi hutoa gesi zaidi za sumu ikilinganishwa na betri ilio na asilimia 50 ya chaji.

WANAFUNZI WA SECONDARY MBEYA WAKIZUNGUMZIA JINSI MWENZAO ALIVYO CHAPWA


Zamalek yasema "uchawi" uliwafanya kushindwa

Zamalek yasema "uchawi" uliwafanya kushindwa

  • 24 Oktoba 2016
     Kocha mkuu Moamen wa Zamalek

Image caption Kocha mkuu Moamen wa Zamalek


Mwenyekiti wa Zamalek Mortada Mansour amelaumu "uchawi na bahati mbaya" kwa kushindwa kwa timu yake mikononi mwa timu ya Afrika Kusini ya Mamelodi Sundowns katika fainali ya ligi kuu barani Afrika.
"Kulikuwa na nafasi nyingi kwetu sisi katika mechi zote, lakini mpira ulikataa kutingiza nyavu" Mansour aliongeza, baada ya kushindwa mabao 3-1 kwa jumla ya mabao.
Pia aliunga mkono kwa kocha Moamen Soliman kusalia katika nafasi yake licha ya kupoteza.
"Tuna wakufunzi wazuri na sitawafuta kazi," amesema Mansour, mbaye aliwatumia wakufunzi sita mwaka huu.
"Kocha Moamen atasalia kama mkufunzi mkuu wa Zamalek, hadi mwisho wa msimu huu."