Labels

Saturday 30 September 2017

UFUGAJI WA SAMAKI

Aina ya samaki wafugwao ni perege, sato ngege, magenge nk. Sababu za kufuga samaki  wa jami hizo ni ;
  1.  Huishi katika maji ya kawadia yenye joto la wastani 
  2. Huzaliana kwa wingi
  3. Hula majani ambayo hupatikana kiraisi majumbani na mashambani 
       MAHITAJI KATIKA UFUGAJI WA SAMAKI

  1. Uchaguzi wa eneo
  2. Uchimbaji wa bwawa
  3. Mbolea na majivu
  4. Uwekaji wa maji
  5. Upendaji wa vifaranga
  6. Usafishaji wa bwawa
      UCHAGUZI WA ENEO

  1. Pasiwe na mteremko mkali
  2. Pawe na udongo unaohifadhi maji
  3. Pawe na maji ya kudumu
  4. Pawe karibu na nyumbani
     UCHIMBAJI WA BWAWA
  1. Safisha eneo kisha lipime kulingana na ukubwa wa mahitaji ya bwawa lako
  2. Pima kingo weka kamba kuonyesha sehemu kingo zako zitakapopita
  3. Chonga sakafu yako chini na  sawazisha kuta zote za juu.
  4. Panda majani ya mudu ili kuzuia mmomonyoko
    UWEKAJI WA MAJIVU NA MBOLEA
 Nyunyizia mbolea ya samadi na majivu katika bwawa lako hakikisha
   UWEKAJI WA MAJI
Jaza bwawa lako maji kwa siku tatu mfululizo kisha yaache yakae kwa siku saba ndipo upade vifaranga wa samaki
   UPANDAJI WA VIFANGARA WA SAMAKI
Samaki bora hutokana na vifaranga bora wa samaki, vifaranga hupandwa asubuhi na husafiri na ndoo za plastiki. Zingatia wingi wa samaki na ukubwa lako la kupanda vifaranga vya samaki kwa kila mita ya mraba moja vifaranga wawili.

No comments:

Post a Comment