Labels

Sunday 23 April 2017

Barcelona waipa kipigo kikali Madrid El Clasico

Lionel Messi akishangilia goli baada ya kuifunga real madrid.

Ma gwiji wa soka wa Hispania klabu ya Barcelona, wameibuka kifua juu katika mchezo wa El Clasico baada ya kuichapa Real Madrid kwa mabao 3-2.


Neema katika lango la Barcelona ilianza kuonekana mnamo baada ya Lionel Messi kusawazisha bao lililo waweka madrid mbele ambalo lilifungwa na kiungo wa kibrazil Henrique Casemiro.


 katika dakika ya 73 Ivan Rakitic aliiongezea Barca goli la pili  kabla ya James Rodriguez mshambuliaji wa Real Madrid  kuchomoa bao katika dakika ya 86.

Katika dakika ya 90 Lionel Messi, aliifungia timu yake bao la ushindi na hivyo timu yake inarejea kilele mwa ligi wakiwa na alama 75 huku madrid wakiwa katika nafasi ya pili kwa alama 75, wakitofautiana idadi ya magoli na Real wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
Madrid walicheza pungufu katika mchezo huu baada ya beki wake kisiki Sergio Ramos, kupewa kadi nyekundU.

Share na wenzako uwezavyo.

No comments:

Post a Comment