Labels

Friday 21 April 2017

Wasanii wa Bongo Movie wanaishi ‘Ki Bongo Flava

Rapa Nikki wa Pili kutoka katika kundi la Weusi amefunguka na kusema kuwa wasanii wengi wa bongo movie wanafahamika kwa mambo mengi na si kufahamika zaidi kutokana na kazi zao za kila siku.
Nikki wa Pili.


Hatua hiyo imekuja baada ya siku ya Jumatano wiki hii baadhi ya wasanii wa filamu nchini kuandamana wakiwa na Mkuu wa Mkoa Dar es salaam, Paul Makonda, kupinga filamu hizo ambapo RC huyo alipiga marufuku filamu hizo huku akitaka wafanyabishara kufuata taratibu za kuziingiza nchini.
Baadhi ya wasanii wa filamu na muziki wamekuwa wakipingana na hatua hiyo ambapo Alhamisi hii, rapa Nikki wa Pili ameamua kutia neno kwenye sakata hilo.
“Nchi zote zilizoendelea zililinda masoko ya nyumbani, ndio tulilinde lakini wenye movie nao wajilinde kwa kujiongeza kila kukicha,” alitweet Niki wa Pili.
“Bongo Movies mwanzoni walikuwa na soko, kuanza ni kujaribu, but ku sustain is a science, mwendelezo wa lolote huitaji maarifa na maisha ya mwigizaji tofauti na mwanamuziki, Denzel na Jiga tofauti, sasa waigizaji wanaishi ki bongo fleva,” aliongeza.

Wasani wengine ambao walipinga maandamano hayo ni pamoja na Steve Nyerere ambaye alikuwa mwenyekiti wa Bongo Movie Unit pamoja na Bella Fasta.

No comments:

Post a Comment