Labels

Tuesday 25 April 2017

Roma yaishusha daraja Pescara Seria A

Wachezaji wa As Roma wakishangilia goli
Klabu ya As Roma ikicheza ugenini katika dimba la Adriatico imeichapa Pescara, kwa mabao 4-1 na hivyo kuishusha rasmi timu hiyo mpaka Seria B.
Pescara wababuruza mkia katika ligi wakiwa na alama 14 huku wakiwa wamecheza jumla ya michezo 33 msimu huu.
Roma walipata magoli yao kupitia kwa viungo wake Kevin Strootman na Radja Nainggolan, huku winga mahiri wa timu hiyo Mmisri Mohamed Salah, akitupia mabao mawili.
Kwa ushindi huo Roma wanapunguza wigo wa alama na vinara wa ligi hiyo Juventus kuwa alama nane baada ya ushindi wa mchezo huu, huku wote wakiwa wamecheza michezo 33.
Mkurugenzi wa mpya wa michezo wa As Roma Ramon Monchi
Wakati huo huo klabbu hiyo ya Roma imemtangaza Ramon Rodriguez 'Monchi' kuwa mkurugenzi wa michezo wa timu hiyo
Monchi alikuwa mkurugenzi wa michezo wa timu ya Sevilla ya Hispania kwa miaka 17 na kuisaidi timu hiyo kuchukua mataji matatu ya Europa ligi.

No comments:

Post a Comment