Labels

Thursday 20 April 2017

EPL: Chelsea na Tottenham zatawala kikosi bora Ligi Kuu Uingereza

Kikosi bora cha Ligi ya Premia 2017
Chelsea na Tottenham zimetawala kikosi cha wachezaji 11 bora wa Ligi ya Premia msimu huu ambacho kimetangazwa na Chama cha Wachezaji wa Soka ya Kulipwa Uingereza.
Klabu zote mbili zina wachezaji wanne katika kikosi hicho.
Mabeki Gary Cahill na David Luiz pamoja na viungo wa kati N'Golo Kante na Eden Hazard ndio wachezaji wa Chelsea waliojumuishwa kwenye kikosi hicho.
Tottenham inawakilishwa na mabeki Kyle Walker na Danny Rose, kiungo wa kati Dele Alli na mshambuliaji Harry Kane.
Mlindalango wa Manchester United David de Gea, Sadio Mane wa Liverpool na mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku pia wamo kwenye kikosi hicho.
Kikosi bora cha msimu huu katika Ligi ya Daraja la Pili pia kimetangazwa ambapo wachezaji wanne wa klabu iliyopandishwa daraja hadi Ligi Kuu ya England, Brighton wakiwa kwenye kikosi hicho.Kwa maelezo zaidi bonyeza hapa

PFA Championship 2017

1 comment: