Labels

Monday 24 April 2017

Kylian Mbappe arejesha Monaco kileleni Ufaransa

Kylian Mbappe amefunga mabao 23 mashindano yote msimu huu
Chipukizi Kylian Mbappe alifunga bao la ushindi na kuwawezesha Monaco kulaza Lyon na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Ufaransa, Ligue 1 mnamo Jumapili.
Radamel Falcao alikuwa amefungia wageni hao bao la kwanza lakini likakombolewa na Lucas Tousart aliyefungia Lyon bao kwa kichwa.

Lakini Mbappe, 18, alifunga bao lake la 13 ligini msimu huu na kuwaongezea Monaco matumaini ya kushinda taji lao la kwanza la ligi tangu 2000.
Monaco wanatoshana nguvu kwa alama na Paris St-Germain, lakini wako mbele kwa mabao.
Aidha, wana mechi moja hawajacheza.

No comments:

Post a Comment